Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kibiti kimeagiza Wakala wa Maji vijijini RUWASA Wilaya ya Kibiti na Wakandarasi wanaojenga miradi ya maji kutekeleza miradi ya maji wilayani humo kwa wakati na kwa ubora waliokubaliana kwenye mikataba ya Kazi ili harakisha ufikishaji wa huduma ya maji kwa Wananchi kwa wakati na kumaliza adha ya kukosa maji wilayani humo.
Akizungumza wakati akiwa kwenye ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya CCM wilayani Kibiti Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibiti Juma Ndaruke amesema wamejiridhisha kwa kazi nzuri na kubwa iliyofanyika na serikali kupitia Wakala wa Maji vijijini RUWASA Wilaya ya Kibiti inayoongozwa na Meneja Eng. Ramadhani Mabula.
Ndaruke amesema Wakandarasi waheshimu mikataba iliyosainiwa baina ya RUWASA na Wakandarasi wa miradi katika kufikisha huduma ya maji kwa Wananchi wilayani humo.
Amesema serikali imewekeza zaidi ya shilingi milioni 900 ili kuhakikisha Wananchi wa vijiji na vitongoji vya Wilaya ya Kibiti vinapata huduma ya maji safi na salama katika muda sawa na mikataba iliyosainiwa.
Aidha Kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Kibiti imeonyesha kuridhishwa na hatua za utekelezaji wa miradi ya maji wilayani humo na kusema utekelezaji huo utawasaidia CCM katika kuwanadi Wagombea wa chaguzi za serikali za mitaa na vitongoji mwaka huu na uchaguzi Mkuu mwakani.
Ndaruke amesema hatua za utekelezaji huo utawasaidia kurahisisha ushindi wa kishindo kwa CCM kwa kuufanya chaguzi kuwa rahisi sana mwakani kwani CCM ilichoahidi kwa Wananchi katika uchaguzi Mkuu uliopita kwa upande wa miradi ya maji imetekeleza.
Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa fedha zaidi ya shilingi bilioni 3.5 za kutekeleza miradi ya maji wilayani Kibiti.
Meneja wa Wakala wa Maji vijijini RUWASA Wilaya ya Kibiti inayoongozwa na Meneja Eng. Ramadhani Mabula amesema utekelezaji wa miradi ya maji wilayani Kibiti inaendelea katika hatua mbalimbali za utekelezaji wake ili kuwafikishia maji ya bomba nyumbani Wananchi wa Wilaya hiyo.
Eng. Mabula amesema Wilaya hiyo RUWASA katika kuwahidimia Wananchi Wilaya ya Kibiti wanadaiwa maji lita milioni 11 kwa siku lakini kwasasa wanazalisha maji lita milioni 8 kwa siku.
+++++