Home Michezo ROBO FAINALI YA KWANZA MATHAYO CUP KUPIGWA KESHO, KITAJI FC DHIDI YA...

ROBO FAINALI YA KWANZA MATHAYO CUP KUPIGWA KESHO, KITAJI FC DHIDI YA NYAKATO FC

Na Shomari Binda-Musoma

MASHINDANO ya Mathayo Cup yaliyondaliwa na mbunge wa jimbo la Musoma mjini, Vedastus Mathayo,yamefika hatua ya robo fainali.

Bingwa wa mashindano haya ataondoka na zawadi ya ng’ombe,mshindi wa pili ataondoka na shilingi laki 5 na mbuzi,mshindi wa 3 laki 3 na mbuzi pamoja na zawadi nyingine za wachezaji.

Mchezo wa robo fainali ya kwanza hapo kesho kwenye uwanja wa Mara sekondari utazikutanisha timu za Kitaji fc na Nyakato fc ambazo tayari zimeanza tambo nje ya uwanja.

Kocha wa Kitaji fc Zamoyoni Taruma amesema mwaka huu wamedhamiria kuchukua ubingwa wa mashindano hayo.

Amesema kama kocha ameandaa kikosi chake vizuri kwaajili ya mashindano hayo na anapata ushirikiano mkubwa kutoka kwa viongozi wa Kata na wananchi.

Kwa upande wake meneja watimu ya Nyakato fc, Zakayo Zakayo amesema hawajaona timu ya kuwazuia kuchukua ubingwa msimu huu.

Amesema hatua ngumu ilikuwa ni kupita makundi na wamefanya hivyo na kilichobaki ni kuchukua ubingwa na kuupeleka Nyakato.

Wakati huo huo mbunge wa jimbo la Musoma mjini,Vedastus Mathayo,ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha mchezaji Angelo Malima aliyefariki usiku wa kuamkia jana.

Angelo alikuwa mchezaji kiongozi wa timu ya Kata ya Rwamlimi iliyokuwa ikushiriki mashindano hayo na kutolewa katika hatua ya awali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!