Home Kitaifa ROBBI ATOA SOMO UKATILI WA KISIASA KWA WANAWAKE KUELEKEA UCHAGUZI SERIKALI ZA...

ROBBI ATOA SOMO UKATILI WA KISIASA KWA WANAWAKE KUELEKEA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

Na Shomari Binda-Musoma

MJUMBE wa Baraza la Wanawake Tanzania ( UWT) Taifa kutoka mkoa wa Mara Robbi Samwelly amesema ni wakati umefika kwa wanawake kuacha kufanyiwa ukatili wa kisiasa.

Amesema licha ya ukatili wa kimwili,kisaikolojia,kiuchumi na kingono upo ukatili wa kisiasa ambao unaibuka hasa nyakati za uchaguzi.

Akizungumza kwenye kikao cha baraza la wazazi wilaya ya Musoma mjini kilichofanyika leo agosti 20 kwenye ukumbi wa CCM mkoa amesema wapo wanawake wanaoambiwa hawafai kugombea na kudai huo ni ukatili.

Amesema mwanamke kuchafuliwa,kuambiwa hafai kugombea na kutukanwa jukwaani ni ukatili mbaya ambao unapaswa kupingwa.

Robbi amesema kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa baadae mwaka huu jumuiya ya wazazi ya CCM kupitia viongozi na wajumbe wanapaswa kusimama imara kupinga ukatili huo.

Mjumbe huyo ambaye pia ni mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Hope For Girls and Women Tanzania linalojishughulisha na shughuli za malezi kwa wasichana amesema moja ya jukumu lao ni kutoa elimu.

” Nishukuru sana jumuiya ya wazazi wilaya ya Musoma mjini kwa mwaliko walionipa ili kutoa elimu juu ya masuala ya ukatili wa kijinsia.

” Tunalo jukumu kama wazazi licha ya haya mambo ya kisiasa tupinge ukatili wa kijinsia maana leo watoto wanabakwa na kulawitiwa na kuna athari kubwa juu ya ukatili huo”,amesema.

Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi ya CCM Wilaya ya Musoma mjini Eras James amemshukuru Robbi Samwelly kwa ujumbe na somo alilolitoa kwenye baraza hilo.

Amesema wajumbe waliopata elimu hiyo wanapaswa kuishusha kwenye jamii na kuhakikisha kila mmoja anabadilika na kuachana na masuala ya ukatili.

Aidha Mwenyekiti huyo amewataka wajumbe wa baraza la wazazi kuhamasisha uandikishaji daftari la wapiga kura kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!