Na Magrethy Katengu
Baraza la Sanaa la Taifa katika
kuhakikisha kazi zinazofanywa zinajulikana limewachagua Mabalozi watakaofanya kazi ya kulitangaza ndani na nje ya nchi shughuli wanazozifanya ambao ni Bi. Ritha Paulsen (Madam Ritha) na Mrisho Mpoto (Mjomba).
Akizungumza leo na Waandishi wa habari Katibu Mtendaji wa Basata Dkt. Kedmon Mapana amesema kwa mujibu wa mtiririko wa utekelezaji wa shughuli za sanaa nchini Baraza limedhamiria kuwa na mabalozi watakaofanya kazi ya kulitangaza majukumu yake yote wanayofanya ndani na nje ya ncho ili kusaidia kutambulisha kuwa taasisi inayoshughulikia mustakabali wa maendeleo ya wasanii na wadau wa sanaa nchini.
“Mabalozi wetu Hawa watashirikiana na baraza la sanaa la Taifa ili kupanua wigo wa mawazo na kutangaza falsafa yetu iliyojikita katika kufufua zaidi kukuza zaidi na kuendeleza zaidi sekta ya Sanaa na kuipa mawanda mapana ya ubunifu na ushirikiano huu umejikita katika makubaliano ya kufanya kazi kwa muda wa miezu 12 kuanzia leo ambapo tutasaini mkataba wa maridhiano” amesema Dkt. Mapana
Kwa Upande wake Balozi Mrisho Mpoto(Mjomba ) ameshukuru BASATA kumwamini yeye na Madam Ritha kuwapa dhamana hivyo watajitahidi wanakututana na wasanii kurudisha maadili kwenye jamii kwani sasa nyimbo zinazoimbwa zinaendana na tamadani za Kitanzania na kupunguza nyimbo zinazoimbwa wakiwa wamevaa nusu uchi.