Home Kitaifa RIPOTI YA MABADILIKO YA TABIA NCHI NA HAKI ZA BINADAMU YAZINDULIWA JIJINI...

RIPOTI YA MABADILIKO YA TABIA NCHI NA HAKI ZA BINADAMU YAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM

.Na Magrethy Katengu

Mtandao wa Jinsia Elimu Mabadiliko ya Tabia ya nchi Umesema Makundi ya Wanawake,watoto wazee na vijana wa katika kipindi hiki kigumu ambapo mvua hazijanyesha baadhi ya Mikoa ikiwemo Tanga Handeni wanakumbana na changamoto ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji huku Mifugo yao ikifa na wanafunzi kuwa watoro shuleni .

Akizungumza Leo Jijini Dar es salaam Mratibu wa Mtandao wa Jinsia Elimu Mabadiliko ya Tabia ya nchi Jinsia na haki za binadamu Maria Matui katika hafla ya Uzinduzi wa ripoti ya Mabadiliko ya Tabia nchi na haki za binadamu iliyofanyika mwezi Juni -Julai mwaka huu ambao amesema ripoti hiyo ilibaini athari za ukame ambapo imesababisha baadhi ya wanafunzi kutokana na hali hiyo wakati mwingine kukosa shule kwenda kutafuta maji huku wengine wakiacha shule kutafutia wanyama maji .

“Mvua zilinyesha kidogo mwaka huu hivyo kila eneo la nchi liliathirika na mabadiliko ya tabia nchi (Ukame)ambao umeleta athari mbalimbali kwa jamii ikiwemo kukosekana kwa maji,mazao kupatikana kidogo hivyo kuwapa wakati mgumu makundi ikiwemo ya Wanawake hususani kinamama, watoto, kulazimika kutembea umbali mrefu kutafuta maji jambo ambalo husababisha wakumbane na changamoto nyingine za ukatili wa kijinsia “Amesema Matui.

Hata hivyo amesema sababu kubwa zinazosababishwa Mabadiliko ya tabia nchi ni shughuli za kibinadamu ikiwemo ufugaji wanyama wengi eneo moja, Kilimo holela,shughuli za Viwanda,ukataji miti Ovyo,ushavizi katika vyanzo vya maji hivyo ni budi uwepo wa sheria na kanuni zinazoendana sawa, ikiwemo sheria ya ardhi, sheria ya utalii na sheria ya kilimo zikifanya kazi sambamba zitawezesha kuepusha uharibifu wa mazingira na hifadhi asili ambazo hutunza mazingira hususani kufyonza hewa ya ukaa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Youth Survival Organisation Hamphery Mrema amesema bado ushirikishwaji wa vijana ni mdogo katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya Tabianchi ambao ni wengi ni zaidi ya asilimia 60 ya Watanzania ni umri chini ya miaka 35 hivyo wakihusishwa kwenye masuala ya mabadiliko ya Tabianchi watakuwa na mchango mkubwa na kuleta mtazamo chanya

Naye Neema Ndemno Mtafiti na habari Kutoka upande wa Wafugaji amesema akiwa anafanya utafiti wake wakati anafanya mahojiano alikutana na wanawake ambao ni walilalamika kudhalilishwa Kwa kubakwa wakati wakienda kutafuta maji kutokana na baadhi ya wanaume vijana kudamka kuchota maji kabla visima havijakauka hivyo wakiwaomba angalau maji ya kunywa huwaomba rushwa ya ngono ndiyo wawapatie maji

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!