Home Kitaifa REA YAENDELEA NA USAMBAZAJI WA MITUNGI YA GESI YA KILO SITA KWA...

REA YAENDELEA NA USAMBAZAJI WA MITUNGI YA GESI YA KILO SITA KWA BEI YA RUZUKU MKOANI TANGA

📌Mitungi ya gesi ya 26,040 kusambazwa

📌Kila wilaya kupatiwa mitungi ya gesi 3,255

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeingia mkataba na mtoa huduma kampuni ya Manjis Logistics Limited ambaye atahudumia wilaya zilizopo ndani ya Mkoa wa Tanga kwa kuuza kwa bei ya ruzuku mitungi ya gesi ya kilo sita pamoja na vifaa vyake katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji.

Hayo yamebainishwa Machi 01 , 2025 mkoani Tanga na Msimamizi wa mradi kutoka REA, ndugu Abdulrazack Mkomi wakati wa usimamizi na utekelezaji wa mradi wa usambazaji mitungi ya gesi ya kilo sita kwa bei ya ruzuku wilaya ya Muheza mkoani Tanga.

Mkomi amesema kuwa mitungi ya gesi 26,040 itakayosambazwa mkoani Tanga itachochea kwa kiasi kikubwa matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia.

“Lengo la mradi ni kukuza, kuchochea, kuwezesha na kuboresha upatikanaji wa huduma za nishati safi ya kupikia ili kulinda afya za watanzania, kuboresha uchumi na kutunza mazingira ambayo yamekuwa yakiharibiwa kutokana na matumizi ya nishati isiyo safi ya kupikia.

Mkomi ameongezea kuwa, ili kurahisisha matumizi ya nishati safi ya kupikia Serikali imetoa ruzuku kwenye mitungi ya gesi ya kilo sita 3,255 kwa kila wilaya na mwanachi atatakiwa kuwa na kitambulisho chake cha Taifa ( NIDA) pamoja na pesa taslimu shilingi 17,500 tu.

Mkomi amesema, Serikali kupitia REA imetenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ikiwemo gesi (LPG) katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa mji na katika mkoa wa Tanga kiasi cha shilingi milioni 455.7 kimetengwa kutekeleza mradi.

Amezitaja wilaya zitakazonufaika kuwa ni pamoja na Wilaya ya Muheza, Korongwe, Bumbuli, Handeni, Lushoto, Pangani, Kilindi na Mkinga .

Kwa upande wake, Diwani wa kata ya kicheba, Mhe. Khamisi Muhina ameipongeza REA kwa kuja na mradi huo na kuiomba iwe endelevu ili iweze kuwasambazia wananchi wengi nishati hiyo muhimu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!