Home Kitaifa RC MWASSA AUNDA KAMATI KUHAKIKI UPIMAJI ARDHI

RC MWASSA AUNDA KAMATI KUHAKIKI UPIMAJI ARDHI

Na Saidi Ibada, Morogoro

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma mwassa ameunda kamati ya watu 5 ambao watashirikiana na kamishna wa ardhi wa Wilaya ya Mvomero na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kwa lengo la kuhakiki na kupima eneo lenye ekari 5,000 ambalo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliagiza eneo hilo kugawanywa kwa wananchi waishio eneo hilo.

Mhe. Fatma Mwassa ameunda Kamati hiyo Februari 18 mwaka huu wakati wa mkutano wa hadhaara na wananchi waishio eneo la msitu wa kuni wa CCT Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema ameunda kamati hiyo ambayo wajumbe wake ni wananchi waishio katika eneo hilo lengo kuu la kuwashirikisha wananchi hao ni kuhakiki na kupima ekari hizo 5,000 ili kuondoa utata ambao unaweza kujitokeza baadae.

“…na sasa tuna kamati, na hii itatusaidia sana kwenye kutatua changamoto…” amesema Mhe. Fatma Mwassa.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ameiagiza TFS kwenda kung’oa mahindi yao katika eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya uhifadhi wa msitu huo kutokana na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wa eneo hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Judith Nguli amewataka wananchi kutoa kero zao bila woga mbele ya viongozi wao pindi wanapo watembelea ili kutatua kero na changamoto zinazowakabili.

Awali, Bwana Denis Leo mkazi eneo hilo ameilalamikia TFS kwa kuwaondoa katika eneo la hifadhi na wao kulitumia eneo hilo kwa ajili ya kilimo jambo ambalo tayari Mhe. Mkuu wa Mkoa amekwisha litolea maelezo na maelekezo.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!