Home Michezo RC MTANDA MGENI RASMI BONANZA LA KUMBUKUMBU MIAKA 24 YA MWALIMU NYERERE

RC MTANDA MGENI RASMI BONANZA LA KUMBUKUMBU MIAKA 24 YA MWALIMU NYERERE

Na Shomari Binda-Musoma

MKUU wa mkoa wa Mara Saidi Mtanda anataeajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye bonanza la kumbukumbu ya miaka 24 ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Bonanza hilo litafanyika kwa siku 2 oktoba 14 na 15 kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Karume mjini Musoma kuanzia saa 2 asubuhi.

Timu 8 kutoka kanda ya ziwa za veteran kwa michezo ya soka na netball zitashiriki bonanza hilo lililoandaliwa na Musoma veteran.

Mabingwa watetezi wa mwaka jana timu ya Rock City veteran kutoka Mwanza ni moja ya washiriki pamoja na timu za Mwanza veteran,Buswelu veteran,Kishapu veteran,Simiyu veteran,Mara veteran,Biashara United veteran na Musoma veteran.

Mmoja wa waratibu wa bonanza hilo Yohana Mirobo amesema maandalizi yapo kwenye hatua za mwisho na timu zinatarajiwa kuwasili leo jioni.

Amesema bonanza la mwaka huu linaonekana kuwa na ushindani kutokana na kila timu kujiandaa vizuri.

Yohana amesema bado wanapokea michango kutoka kwa wadau ili kuweza kufanikisha bonanza hilo.

“Bonanza litafanyika kwa siku 2 na tumemualuka mkuu wa mkoa wa Mara Saidi Mtanda kuwa mgeni rasmi kwenye bonanza hili”

“Tunawaomba wadau watushike mkono ili tuweze kufanikisha zaidi bonanza hili ambapo tutakuwa na wageni zaidi ya mia tatu”, amesema Yohana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!