Home Kitaifa RC MTANDA AWATAKA WATUMISHI WASIWE VIKWAZO UTOAJI WA TAARIFA

RC MTANDA AWATAKA WATUMISHI WASIWE VIKWAZO UTOAJI WA TAARIFA

Na Shomari Binda-Musoma

MKUU wa mkoa wa Mara Said Mtanda amekutana na Waandishi wa Habari mkoa wa Mara huku akitoa wito kwa watumishi wa umma wasiwe kikwazo cha utoaji wa taarifa.

Akizungumza kwenye kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa uwekezaji kilichowashirikisha maafisa habari kutoka kwenye wilaya zote za mkoa amesema Waandishi ni chachu ya kusukuma maendeleo na wanapaswa kushirikishwa.

Amesema lengo la kukutana ni kuangalia haliyofanyika mwaka huu wa 2023 na changamoto zake na kuona namna ya kwenda pamoja kwa mwaka 2024.

Mtanda amesema mkoa wa Mara unazo rasilimali nyingi ambazo Waandishi wa Habari wanapaswa kuusaidia mkoa kuzitangaza.

Amesema serikali inafanya mambo makubwa chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan hivyo watumishi wasiwe vikwazo ya kutozitoa.

Nashukuru kukutana nanyi siku ya leo kuweza kuzungumza tuliyofanya mwaka 2023 na changamoto zake na kuona tufanye nini 2024 ili kuweza kwenda pamoja.

Nawapongeza kwa kazi zenu nzuri mnazozifanya na endeleeni kuchapa kazi kwa uhuru na kama kuna jambo linakwenda tofauti tuambiane” amesema Mtanda.

Mkuu huyo wa mkoa amewataka Waandishi wa Habari mkoa wa Mara kuandika habari za ukweli na za uchunguzi ili kuweza kuusaidia mkoa.

Aidha amewataka maafisa habari kwenye halmashauri zote kutoa ushirikiano kwa Waandishi wa Habari katika kutekeleza majukumu yao.

Kwa upande wao Waandishi wa Habari walioshiriki mkutano huo wamemshukuru mkuu wa mkoa kwa kuwajali na kuthamini mchango wao.

Wamesema amekuwa ni mkuu wa mkoa wa pekee aliyefungua ukurasa mpya wa mashirikiano ya kufanya kazi kwa pamoja katika kusukuma mbele maendeleo ya mkoa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!