Home Kitaifa RC MTANDA AWAITA WAFANYABIASHARA WAWEKEZAJI KUWEKEZA MKOA WA MARA

RC MTANDA AWAITA WAFANYABIASHARA WAWEKEZAJI KUWEKEZA MKOA WA MARA

Na Shomari Binda- Musoma

MKUU wa mkoa wa Mara Said Muhamed Mtanda amewaita wafanyabiashara na wawekezaji kuwekeza mkoa wa Mara kwani ni salama na una maeneo ya kutosha.

Akizungumza na rais wa chemba ya Wafanyabiashara Kilimo na Viwanda (TCCIA) Vicent Minja ofisini kwake amesema mkoa wa Mara unazo fursa nyingi za uwekezaji zikiwemo za ujenzi wa hotel hivyo wafanyabiashara na wawekezaji waweze kuzitumia.

Amesema mkoa wa Mara hauna vikwazo kwa mfanyabiashara au muwekezaji yoyote anayetaka kuwekeza na wapo tayari kutoa ushirikiano wowote unao hitajika

Mtanda amemuhakikishia rais huyo wa TCCIA kuwa hali ya usalama kwa mkoa wa Mara ni nzuri na mfanyabiashara yoyote atakaye wekeza biashara yake itakuwa salama.

Amesema sekta binafsi ndio injini ya maendeleo na serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa karibu kwenye sekta hiyo kwa kipindi chote

Niwakaribishe sana wafanyabiashara mkoa wa Mara kuja kuwekeza kwa kuwa mkoa ni salama na biashara zenu zitakuwa salama.

Tunazo fursa za uwekezaji nyingi tukihitaji na hotel za kisasa njooni muwekeze na mimi nipo tayari kuwapa ushirikiano njooni muwekeze nyumbani”amesema

Kwa upande wake rais wa Chemba ya Wafanyabiashara, Kilimo na Viwanda(TCCIA) Vicent Minja amesema wito uliotolewa na mkuu wa mkoa ni sahihi na anapaswa kuungwa mkono.

Amesema amepita mkoa wa Mara na kuona fursa zipo nyingi na ardhi ya kutosha yenye rutuba inayofaa hata uwekezaji ya kilimo.

Minja amesema ushirikiano walioupata kwa mkuu wa mkoa ni mzuri na TCCIA ipo tayari kutoa ushirikiano ili kuinua uchumi.

Akizungumza na wafanyabiashara wa mkoa wa Mara ametoa wito kwa wafanyabiashara kujiunga na chemba ili kuwa na nguvu ya pamoja ya kutekeleza majukumu.

Amesema zipo fursa nyingi ambazo wafanyabiashara wanazipoteza ikiwa hata kusaidiwa masuala ya TRA kwa kuwa mmoja mmoja.

Katika ziara ya rais huyo wa TCCIA licha ya kuzungumza na mkuu wa mkoa na wafanyabiashara ametembelea shughuli mbalimbali za wafanyabiashara, kilimo na viwanda na kutoa ushauri wa kuinua shughuli zao

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!