Home Kitaifa RC MTANDA ATOA MAAGIZO KWA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI KUWAPA MAFUNZO WAKULIMA

RC MTANDA ATOA MAAGIZO KWA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI KUWAPA MAFUNZO WAKULIMA

Na Shomari Binda-Musoma

MKUU wa mkoa wa Mara Said Mtanda ametoa maagizo kwa wakurugenzi wa halmashauri zote za mkoa kuwasaidia wakulima kupata mafunzo.

Maagizo hayo yametolewa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya ya Rorya Juma Chikoka wakati akifunga maonyesho ya siku 3 ya kilimo mseto.

Maonyesho hayo ya 8 yaliyoandaliwa na shirika la Vi-Agroforestry yaliyoendana na miaka 40 ya ufanyaji kazi wake Afrika Mashariki yamefanyika kwenye kituo cha mafunzo kilichopo Bweri manispaa ya Musoma.

Amesema wakurugenzi kwenye halmashauri wanapaswa kutenga muda wa kuwapa mafunzo wakulima ili kuwafanya kulima kilimo chenye tija.

“Nimekuja hapa kwa niaba ya mkuu wetu wa mkoa ambaye alipaswa kuwa mgeni rasmi wetu na yupo kwenye majukumu mengine”

“Haya ntakayoyasema ni maneno yake ambayo ameyaandika kwenye hutuba yake ya kufunga maonyesho haya ya 8 ya kilimo mseto” amesema Chikoka.

Amesema maafisa ugani wanapaswa kuwatembelea wakulima mashambani na kuwapa elimu na kuandaa mafunzo ya pamoja yakisimamiwa na wakurugenzi.

Kupitia maonyesho hayo amelishukuru shirika la Vi-Agroforestry kwa kuunga mkono juhudi za serikali katika kuwainua wakulima.

Amesema mkoa utayafanyia kazi mapendekezo ya wakulima waliyoyatoa kupitia maonyesho hayo ikiwemo kutembelewa na uhakika wa upatikanaji wa pembejeo.

Baadhi ya wakulima walioshiri maonyesho hayo wamemshukuru mkuu wa mkoa kwa mtazamo wake wa kuwasaidia kuwa na mafunzo ya mara kwa mara ili kuinua kilimo chao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!