Home Afya RC MTANDA ATAKA UWAJIBIKAJI WA VIONGOZI KUINUA AFUA ZA LISHE

RC MTANDA ATAKA UWAJIBIKAJI WA VIONGOZI KUINUA AFUA ZA LISHE

Na Shomari Binda-Musoma

MKUU wa mkoa wa Mara,Said Mtanda, amewataka viongozi katika ngazi za wilaya na mkoa kuwajibika kwenye majukumu yao katika kuinua afua za lishe.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa kikao cha kufanya tathimi ya utekelezaji wa mkataba wa hali ya lishe kwa mkoa wa Mara kilichowashirikisha viongozi kutoka wilaya zote.

Amesema kila mmoja wakiwemo maafisa lishe wanapaswa kufanya kazi ikiwemo kuhakikisha ajenda ya lishe inakuwepo kila mkutano.

Mtanda amesema kuwa na kikao cha ajenda moja ya lishe ni vigumu hivyo ni muhimu kushirikiana na viongozi wengine ikiwa ni pamoja na kuhudhuria vikao vya madiwani na kutoa elimu

Amesema katika kipindi cha mwaka jana mkoa wa Mara ulishika nafasi ya mwisho kitaifa katika hali ya lishe na kusema hali hiyo haiwezi kukubalika.

Kutokuwa na lishe bora kunapelekea utapiamlo kwa watoto na kuwafanya kudhoofika afya na hata kufanya vibaya kwenye masomo.

Mkuu huyo wa mkoa amewataka maafisa lishe kuwa na ushirikiano na wakuu wa wilaya na wakurugenzi ili waweze kutekeleza majukumu yao.

Amesema suala la utoaji utengaji na utoaji wa fedha kwaajili ya utekelezaji wa masuala ya lishe ikiwemo mikutano ufanyike ili kuondoa vikwazo.

Naomba wakuu wa wilaya tushiriki kikamilifu na halmashauri ndio watekelezaji na kutenga fedha kwaali ya kufanya tafiti na kuboresha hali ya lishe na kuleta hali bora”amesema.

Wakizungumza kwenye kikao hicho,maafisa afya kutoka wilaya zote za mkoa wa Mara wamedai kwenda kufanya kazi kwa kujituma zaidi kwa kutekeleza majukumu yao.

Wakuu wa wilaya na wakurugenzi wameahidi kwenye kikao hicho kwenda kuwapa ushirikiano maafisa lishe waweze kutekeleza majukumu yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!