Na Shomari Binda-Musoma
MKUU wa Mkoa wa Mara Said Mohamed Mtanda amepongeza ushindi wa timu ya Biashara United wa mabao 2-0 dhidi ya Copco ya jijini Mwanza.
Mtanda amewaongoza mashabiki wa timu hiyo kuishangilia na kuibuka na pointi 3 muhimu kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Karume mjini Musoma
Akizungumza mara baada ya mchezo huo kumalizika amesema wachezaji wanastahili pongezi kwa kuwa wamepambana kutafuta matokeo hayo.
Amesema ligi ya Championship ni ngumu na matokeo ya pointi za mapema yanahitajika ili kuweza kutafuta nafasi ya kupanda ligi kuu msimu ujao.
Mtanda amesema kumalizika kwa mchezo huo ni maandalizi ya mchezo ujao dhidi ya Pamba utakaochezwa kwenye uwanja huo wa Karume.
Mkuu huyo wa mkoa amewataka mashabiki kuendelea kujitokeza kwa wingi uwanjani kuipa sapoti ya kuishangilia timu yao
Aidha RC Mtanda amesema serikali ya mkoa itaendelea kutoa sapoti kwa timu ya Biashara United ili malengo ya kurejea ligi kuu msimu ujao.
“Niwapongeze sana vijana kwa kupambana na kushinda mchezo huo na sasa tujipange kwa mchezo ujao”
“Tutaendelea kutoa sapoti kama serikali ya mkoa na kupitia wadau mbalimbali ili tufanikiwe kurejea ligi kuu msimu ujao”, amesema