Home Michezo RC MTANDA APONGEZA USHINDI WA BIASHARA UNITED DHIDI YA MBEYA CITY

RC MTANDA APONGEZA USHINDI WA BIASHARA UNITED DHIDI YA MBEYA CITY

Na Shomari Binda-Musoma

MKUU wa mkoa wa Mara Said Muhamed Mtanda amepongeza ushindi wa timu ya Biashara United kwenye mchezo wa Championship.

Biashara United iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City kwenye mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Mkuu huyo wa mkoa ambaye ni mpenzi mkubwa wa michezo amesema amepokea matokeo hayo kwa furaha na kuwapongeza wachezaji na benchi la ufundi kwa ushindi huo.

Amesema mkoa upo pamoja na timu hiyo kwenye ushiriki wake wa ligi ya Championship ili kuendelea kuitafuta nafasi ya kupanda ligi kuu.

Mtanda amesema maelekezo yake aliyoyatoa ya kurekebishwa kwa uwanja wa Karume yanaendelea kufanyiwa kazi ili timu hiyo irejee kuutumia kama uwanja wake wa nyumbani.

Amesema kwa sasa eneo la kuchezea lipo vizuri na maeneo mengine yapo sawa tayari kwa uwanja huo kuendelea kutumika.

“Nawapongeza wachezaji na benchi la ufundi kwa kupambana kule Mwanza na kupata matokeo kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City”

“Uwanja wetu unaendelea kukaa vizuri ili michezo inayofuatia timu irejee nyumbani na mashabiki waweze kuona burudani” amesema Mtanda.

Wakati huo huo kocha wa timu ya Biashara United Amani Josia amewashukuru wanachama na mashabiki wa timu hiyo waliosafiri hadi jijini Mwanza kwenda kuipa sapoti timu yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!