Na Shomari Binda – Musoma
MKUU wa mkoa wa Mara Said Mtanda amemwakilisha Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwenye iftar na jamii mkoa wa Mara.
Iftar hiyo imefanyika kwenye viwanja vya Ikulu ndogo mkoani Mara na kuhudhuriwa na wananchi na viongozi mbalimbali wakiwemo wa dini.
Amesema shughuli hiyo ni ya Rais Dkt.Samia na wanamuwakilisha katika kukutana na jamii katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Mtanda amesema katika kufanikisha jambo hilo la Rais ndio sababu wamefika wasaidizi wake kutoka Ofisi ya Rais Ikulu kujumuika na wananchi.
Amesema katika iftar hiyo Rais Samia ametoa ng’ombe kama kitoweo na sehemu imekwenda kwa wajane kwa matumizi ya nyumbani.
“Shughuli hii ya iftar ni ya mheshimiwa Rais na tupo hapa kwaajili ya kumwakilisha katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan.
“Kwa kutambua hili ni jambo la kwake wapo hapa wasaidizi wake kutoka Ofisi ya Rais Ikulu tukishiriki nao kwa pamoja.
Amesema kupitia Shekh wa Wilaya ya Musoma watafikishiwa wajane sehemu ya swadaka iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kupitia tukio hilo lililopewa jina ” Iftar na Rais Samia“
Wananchi na viongozi walioshiriki wamemshukuru Rais Samia kupitia mkuu wa mkoa Said Mtanda kwa kukutana na kufanya iftar ya pamoja.