Home Kitaifa RC MTANDA AFANYA MIKUTANO CHINI YA MITI KUSURUHISHA MGOGORO WA ARDHI

RC MTANDA AFANYA MIKUTANO CHINI YA MITI KUSURUHISHA MGOGORO WA ARDHI

Na Shomari Binda-Musoma

MKUU wa mkoa wa Mara,Saidi Mtanda, amefanya mikutano na wananchi wa vijiji vya Romng’oroli wilayani Serengeti na Mikomarilo wilayani Bunda ili kumaliza mgogoro uliodumu zaidi ya miaka 40.

Mikutano hiyo imefanyika kwenye vijiji hivyo chini ya miti huku wananchi wakipewa nafasi ya kusikilizwa namna bora ya kutatua mgogoro huo.

Akizungumza na wananchi hao kwa nyakati tofauti,mkuu huyo wa mkoa amesema kamwe mgogoro huo hautamalizika kama hakutakuwa na meza ya mazungumzo.

Amesema watakaoamua mgogoro huo umalizike ni wananchi wenyewe pale watakapo kaa chini.na kuamua kusuruhisha.

Mtanda amesema ameamua kukutana kwa wananchi wa pande zote mbili kupitia viongozi wakiwemo wa serekali ya vijiji na wawakilishi wa wananchi ili kuzungumza.

“Kwa sasa mipaka ile iliyowekwa awali tutaendelea kuitambua wakati tunapoendelea kufanya utaratibu wa kukutana ili kumaliza jambo hili”

“Wapo watu ambao wapo nje ya mkoa wa Mara ambao wanachochea mgogoro huu na tutafatilia tuone namna ya kushughulika nao na wale wanaodaiwa kumiliki maeneo tutawaita kwenye kamati ya mazungumzo na kuhojiwa” Amesema Mtanda

Mkuu huyo wa mkoa amesema hakuna mtu atakayevumiliwa kutaka kufanya uvunjifu wa amani kupitia mgogoro huo na kudai yeye ni mbobezi wa kutatua migogo hivyo hata huo utamalizika.

Amesema wapo viongozi wengi walio ufatilia mgogoro huo zaidi ya miaka 40 lakini ni dipromasia ndio itakayotumika kuumaliza.

Baadhi ya viongozi na wananchi waliohudhuria mikurano hiyo wamemshukuru mkuu wa mkoa kwa kuamua kufanya utaratibu wa kukaa meza ya mazungumzo ili kuweza kutatua mgogoro huo.

Wamesema mgogoro huo unapelekea kutokufanyika kwa shughulu za kiuchumi hivyo kumalizika kwake kutawasaidia kufanya shughuli hizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!