Na Shomari Binda-Musoma
MKUU wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi ametoa wito kwa wananchi kutumia soko la hisa la kampuni ya umma ya HAIPPA PLC Tanzania Limited kujiinua kiuchumi.
Wito huo ameutoa leo januari 30 alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa kampuni hiyo uliofanyika kwenye ukumbi wa MCC mjini Musoma.
Akisoma hotuba kwa niaba yake Katibu Tawala Msaidizi Biashara na Uwekezaji Gambales Timotheo amesema serikali mkoa wa Mara unayo imani na shughuli za HAIPPA.
Amesema HAIPPA imekuwa na uwazi kwenye ufanyaji kazi wa shughuli zao na kwa sasa hakuna uwekezaji mkubwa kama wa kuweka hisa.
Mtambi amesema HAIPPA ni mdau mkubwa wa maendeleo mkoani Mara na kuendelea kuwa balozi wa kuutangaza vyema
mkoa.
Amesema hakuna biashara kubwa kufanya uwekezaji kama kwenye masoko ya hisa kwa kuwa zina tabia ya kupanda na kutoa gawio kwa wana hisa.
” Hakuna sehemu nzuri ya kuwekeza kama kwenye masoko ya hisa na HAIPPA imekuja kama mkommbozi hivyo nitoe wito kwa wananchi wa mkoa wa Mara kujiunga na HAIPPA na kufanya uwekezaji
” Serikali ya mkoa ipo tayari kutoa ushirikiano kwa HAIPPA ili malengo yaliyokusudiwa yaweze kufanikiwa ikiwa ni pamoja na wananchi kuinuka kiuchimi”,imesema sehemu ya hotuba hiyo.
Awali akitoa utambulisho wa HAIPPA mkurugenzi wa kampuni hiyo Boniphace Ndengo amesema lengo namba moja ni kuwafikia watanzania milioni 20 na kuwaelimisha kuhusu uwekezaji.
Amesema lengo namba 2ni kuwawezesha watanzania milioni 6 kuwa na akaunti za uwekezaji,kushiriki mkubwa wa miradi ya PPP na kukuza.kipato chao kutoka wastani wa shilingi milioni 3,000,000 hadi milioni 30,000 000 na kuwezesha kampuni za umma 10 hadi 50 ifikapo mwaka 2035.
Licha ya kushirikisha wana hisa mkutano huo umewashirikisha pia wenyeviti na watendaji wa mitaa kwa lengo la kwends kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kuwekeza kwenye hisa