Home Kitaifa RC MTAMBI AZINDUA UANDIKISHAJI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA NA KUWAITA WANANCHI KUJITOKEZA...

RC MTAMBI AZINDUA UANDIKISHAJI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA NA KUWAITA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI

Na Shomari Binda-Musoma

MKUU wa mkoa wa Mara leo oktoba 11 amezindua zoezi la uandikishaji orodha ya wakazi kwenye daftari la wapiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

Zoezi hilo amelizindulia kwenye kituo cha ofisi ya Kata ya Mukendo na kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha.

Amesema mkoa wa Mara umekuwa ukifanya vizuri kwenye masuala mbalimbali na kuwahamasisha kufanya vyema pia kwenye zoezi hilo.

Mkuu huyo wa mkoa amesema wananchi wasichanganye zoezi hili na ule uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa kuwa ni tofauti.

Amesema uandikishaji uliopita wa daftari la kudumu la wapiga kura na vitambulusho vilivyotolewa ni kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwaajili ya Rais, wabunge na madiwani.

Rc Mtambi amesema zoezi lililoanza leo oktoba 11 hadi 20 ni kwaajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa,vijiji na vitongoji pamoja na wajumbe wao.

” Niendelee kuwakumbusha uandikishaji huu na ule uliopita ni tofauti hivyo wananchi nawahamasisha wajitokeze kwa wingi.

” Mara ni watu wa kufanya vizuri na nawaomba kwenye jambo hili twende tukafanye vizuri uandikishaji ufanikiwe”,.

Afisa uchaguzi manispaa ya Musoma Deus Nyakiriga amesema kwa upande wao wameandaa vituo104 na matokeo ni kuandikisha watu 92,044.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!