Home Kitaifa RC MTAMBI ACHANGIA UJ̌ENZI MSIKITI WA KIGERA BONDENI NA KUTOA UJUMBE WA...

RC MTAMBI ACHANGIA UJ̌ENZI MSIKITI WA KIGERA BONDENI NA KUTOA UJUMBE WA UPENDO

Na Shomari Binda_MUSOMA

MKUU wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi amesisitiza upendo kwa waumini wa dini ya kiislam na jamii kuwa na ushirikiano.

Kauli hiyo imetolewa kwa niaba yake na kaimu Katibu wa Baraza la Waislam Tanzania (Bakwata) Wilaya ya Musoma Juma Masiroli kwenye Maulid ya Msikiti wa Kigera bondeni uliopo manispaa ya Musoma

Amesema hakuna jambo kubwa na bora kama upendo kwenye jamii suala lìnalopelekea kukaa pamoja na kusaidiana mambo mbalimbali

Ujumbe huo wa mkuu wa mkoa kuhusu upendo umeambatana na kuchangia nondo 20 kwenye zoezi la kuchangia ukamilishaji wa upanuzi wa ujenzi wa Msikiti wa Kigera bondeni.

” Mkuu wa mkoa Kanali Mtambi yupo pamoja nasi na anawasalimia na kesho saa 3 asubuhi anawaalika kwenye uwanja wa Mara sekondari kushiriki maombi ya kuliombea Taifa letu.

” Kwenye shughuli ya ujenzi wa upanuzi wa Msikiti wetu wa Kigera bondeni atatuchangia nondo 20 katika makusanyo ya kukusanya vifaa vya ujenzi”amesema Juma.

Sheikh wa Wilaya ya Musoma Abubakar Mkama amemshukuru mkuu wa mkoa na kusema wameupokea ujumbe wake kwa mikono miwili na kuwataka waumini kuufanyia kazi ujumbe wake juu ya upendo.

Amesema palipo na upendo kuna amani na mashirikiano na kufanya kazi kwa kushirikiana jambo linalohitajika kwenye jamii inayoishi pamoja.

Katìka kisomo hicho cha Maulid Sheikh Abuu ameongoza harambee na kupata mifuko ya saruji 63,nondo 42 pamoja na fedha kiasi cha shilingi 8,20000

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!