Home Kitaifa RC MPYA MANYARA, AITEMBELEA WILAYA YA MBULU

RC MPYA MANYARA, AITEMBELEA WILAYA YA MBULU

Ikiwa ni siku moja tu baada ya kuwasili mkoani Manyara kuyaanza majukumu yake. Mkuu mpya wa mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Sendiga amefanya ziara fupi ya kuitembelea wilaya ya Mbulu.

Katika ziara hiyo Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ametembelea Kata ya Balgish na kukagua hatua ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa shule ya Msingi itakayo gharimu thamani ya shilingi Milioni miatatu na arobaini na nane.

Mheshimiwa Mkuu wa mkoa ametumia fursa hiyo kuzungumza na wananchi na kuwaeleza dhamira ya Serikali ya kuendelea kusogeza na kuimarisha huduma, pamoja na kujenga miradi bora itakayo jenga ustawi wa jamii.

Pamoja na mambo mengine Mheshimiwa Mkuu wa mkoa, amewapongeza viongozi na wananchi wa wilaya ya Mbulu kwa umoja na mshikamano, na usimamizi bora wa miradi ya maendeleo. Aidha Mheshimiwa Mkuu wa mkoa amewaomba Wananchi ushirikiano wa kutosha katika majukumu yake ya kuwatumikia wananchi wote wa mkoa wa Manyara.

Akimkaribisha Mkuu wa mkoa katika ziara hiyo, Mkuu wa wilaya ya Mbulu, Kheri James amemueleza Mheshimiwa Mkuu wa mkoa kuwa wilaya ya Mbulu iko shwari, na inaendelea vyema katika kusimamia miradi ya maendeleo, Kutoa huduma kwa wananchi, kukusanya mapato, kusikiliza na kutatua kero za Wananchi na kusimamia utawala wa sheria.

Mheshimiwa Queen Sendiga ameteuliwa kuwa Mkuu wa mkoa mpya wa Manyara akitokea mkoa wa Rukwa,akichukua nafasi ya Mheshimiwa Charles Makongoro Nyerere alie teuliwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Rukwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!