Home Kitaifa RC MAKONDA ATAKA ONGEZEKO LA THAMANI KWENYE BIDHAA ZA KILIMO

RC MAKONDA ATAKA ONGEZEKO LA THAMANI KWENYE BIDHAA ZA KILIMO

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ameiagiza Halmashauri ya Meru Wilayani Arumeru kubuni mpango wa kuwezesha ujenzi wa viwanda vya kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo ili kuongeza tija kwa wakulima na wafugaji wanaopatikana wilayani humo.

RC Makonda , ametoa kauli hiyo leo wakati alipofika kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru na kuzungumza na watendaji wa Wilaya hiyo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya Kikazi ya kutembelea Wilaya zote sita za mkoa wa Arusha.

Akizungumza na viongozi mbalimbali, RC Makonda amewaambia watumishi wa Halmashauri hiyo kuwa sifa kuu ya Kiongozi inapaswa kuwa ya kuwaondoa wananchi kwenye umaskini na kuwapa fursa nyingi zaidi za kuweza kujishughulisha na uzalishaji mali kwa maslahi yao binafsi na ya Taifa.

Akitilia mkazo suala hilo, RC makonda ameiagiza Halmashauri hiyo pia kutafuta mazao ya kimkakati yatakayoitambulisha wilaya hiyo akishauri nguvu kuwekezwa kwenye kilimo cha mazao yanayotumika kwenye kutengeneza marashi kwani tafiti zinaonesha kuwa ardhi ya Wilaya ya Arumeru inafaa kwa kilimo hicho.

Katika mazungumzo yake na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw. Jeremia Kishili, RC Makonda pia ameagiza kuundwa kwa mkakati maalum wa kuvutia sekta na watu binafsi kuwekeza kwenye nyumba za kulala wageni na watalii mbalimbali hasa kwa wale wanaotumia uwanja wa ndege wa Kilimanjaro kuingia nchini Tanzania.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!