Home Kitaifa RC MAKALLA ATOA WITO KUSHIRIKI TAMASHA LA UTAMADUNI

RC MAKALLA ATOA WITO KUSHIRIKI TAMASHA LA UTAMADUNI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amosi Makala ametoa wito kwa watanzania kutambua, kuthamini na kuendeleza urithi na Utamaduni waliorithi kutoka kwa wazazi na kuenzi lugha ya kiswahili

Wito huo ameutoa leo jijini Dar es salaam wakati akitolea ufafanuzi juu ya tamasha la Utamaduni la kwanza kitaifa pamoja na siku ya kiswahili Duniani itakayoadhimishwa julai 1-7 mwaka huu tukio hilo Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa ndiye mgeni rasmi anayetarajiwa kulifungua katika Viwanja vya Uhuru likiwa kimebeba kauli mbiu “Utamaduni wetu; Fahari yetu; tujiandae kuhesabiwa kazi iendelee”

Hata hivyo amesema kuandaliwa Kwa Tamasha hilo ni utekelezaji wa maagizo ya Mhe Rais Samia Suluhu Hassani aliyoyatoa Mkoani Mwanza Septemba 8 katika Tamasha la Utamaduni Mwanza ambapo aliagiza matamasha yafanyike Kwa mzunguko kila Mkoa na washindi wapatiwe tuzo.

Sanjari na hayo alisema kutakuwa na matukio mbalimbali ikiwemo julai 1-3 Usiku wa tarabu katika fukwe za coco Beach ikihusisha wasanii nguli Khadija Kopa, Isha Mashauzi, Patricia Hilary na vikundi kutoka Safina Modern Taraabu, First Class, Nakshi Nakshi pamoja Vikundi kutoka nje ya Nchi za Burundi, Kenya na Visiwa vya Comoro

Sambamba na hayo baada ya julai 4 kutakuwa na maandamano ya Amani kutoka Temeke mwisho hadi uwanja wa Uhuru ambayo yatahusu lugha ya kiswahili na utoaji wa haki na yakiongozwa na Waziri wa katiba na Sheria Mhe Dkt Damasi Ndumbaro

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Lugha kutoka Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo Dkt Mnata Resani alisema Siku ya Julai 6 kutakuwa na kongamano linalohusu mchango wa kugha ya Kiswahili katika harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika na mchokoza mada Balozi Mstaafu Ame Mpungwe pamoja na viongozi kutoka nje ya Nchi

“Kama mnavyofahamu UNESCO imeipa lugha ya kiswahili heshima kwa kuipa siku yake ya kuiadhimisha ambayo ni julai 7kila mwaka hivyo Tanzania ambayo ndiyo yenye Johari hii kiswahili imeandaa Maadhimisho ya siku ya kiswahili Duniani (MASIKIDU) itaadhimishwa mara ya kwanza Duniani”alisema Dkt Mnata

Dkt Mnata alisema katika siku hiyo ya Julai 7 mwaka huu Kwa mara ya kwanza siku ya kiswahili kuadhimishwa duniani huku Tanzania tukio linatarajiwa kufanyika katika Viwanja vya Uhuru Dar es salaam na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Mhe Samia Suluhu Hassani

Pia alisema kiswahili ni lugha pendwa na imekuwa ikizidi kuenea Duniani kote hivyo baraza la kiswahili limekuwa na utaratibu wa kuwatambua wataalamu wa lugha hiyo Kwa kuanzisha kanzi data ili wajisajili lengo ni kujua takwimu yao

Aidha Wananchi wote wanaalikwa kushiriki katika matukio hayo ya kihistoria na Wageni kutoka nje ya nchi watakuwepo kuja kuunga mkono siku ya kiswahili duniani huku Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe Joachim Chisano ,Rais wa Namibia Mhe Sam Nujoma

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!