Mkuu wa Mkoa wa Mwanza CPA Amos Makala ameupongeza uongozi wa Mary Pius Chatanda, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania jinsi ambavyo umejidhatiti kuwajengea uwezo Viongozi Wanawake kutoka makundi mbalimbali.
Hayo yamebainika baada ya Chatanda kutembelea Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mwanza akiwa katika ziara ya Siku moja Mkoani humo. Mhe. Makala amesema, anaiona UWT madhubuti iliyojidhatiti na mikakati endelevu katika kuwakwamua wanawake. Hivyo anafarijika kuona UWT imewezesha mafunzo kwa viongozi wanawake.
Kadhalika, Chatanda akiwa ofisini hapo amesema, yupo Mkoani Mwanza kwa ajili ya mafunzo maalumu ya uongozi kwa viongozi wanawake wa Mikoa 9 ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Ziwa Magharibi ili kuwajengea uwezo wa kujikwamua kiuchumi na kijamii.
Chatanda ameambatana na Katibu Mkuu UWT Ndugu Jokate Mwegelo, Naibu katibu Mkuu UWT Bara, Riziki Kingwande, na viongozi mbalimbali kutoka mikoa ya Mwanza, Geita, Kigoma na Mara pamoja na Mhe. Amina Makilagi Mkuu wa Wilaya Nyamagana