Home Kitaifa RC KUNENGE APOKEA MSAADA WA MAGARI KUMI YA JWTZ, KUHUDUMIA WAATHIRIKA WA...

RC KUNENGE APOKEA MSAADA WA MAGARI KUMI YA JWTZ, KUHUDUMIA WAATHIRIKA WA MAFURIKO RUFIJI NA KIBITI

Na Scolastica Msewa, Rufiji
Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amepokea Msaada wa magari kumi kutoka jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya shughuli za kusafirisha chakula kwenda kwenye makambi ya Waathirika wa mafuriko ya mto Rufiji katika wilaya za Rufiji na Kibiti.

Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa kupokea magari hayo huko Ikwiriri wilayani Rufiji mkoani Pwani Kunenge alisema wamepata misaada ya vyakula lakini kulikuwa na changamoto ya usafiri kutokana na miundombinu kuharibiwa na mafuriko yanayoendelea katika wilaya hizo za Rufiji na Kibiti.

Alimshukuru Amiri jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Ulinzi, Mkuu wa Majeshi General Mkunda kwa Msaada huo wa magari kumi na Maafisa 14 miongoni mwao kuna mafundi ambayo yatasaidia kusambaza chakula kwa walengwa ambao ni Waathirika wa mafuriko ya mto Rufiji.

“Kwa sababu mnafahamu tunapata misaada ya vyakula lakini tulikuwa na changamoto ya usafiri kutokana na changamoto ya Barabara lakini magari hayo yatasaidia kupita kwenye maeneo kama hayo”

Aidha Kunenge alisema magari hayo yatagawanywa kwa wilaya zote mbili zilizoathiriwa na mafuriko hayo za Rufiji na Kibiti ambapo wilaya ya Rufiji itapewa magari saba na wilaya ya Kibiti itapewa magari matatu kwa kuanzia baadae wanaweza kufanya msawazo kulingana na mahitaji ya wilaya hizo mbili baada ya kufanya tathimini ya kuangalia mahitaji jinsi yalivyo sio lazima yakae upande mmoja bali wataangalia mahitaji jinsi yalivyo na jinsi ya kutumia Msaada huo.

Mkuu huyo wa mkoa alikabidhi magari hayo yote kumi kwa Mkuu wa wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele kwa niaba ya wilaya yake ya Rufiji na kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo na kusema jeshi hilo limeshatoa misaada mbalimbali kwa Waathirika hao wa mafuriko lakini pia wataleta tena boti kwaajili ya kusafirisha vyakula kwenda visiwani na maeneo yanayohitaji usafiri wa kwenye maji.

“Walikwishatuletea vifaa na wao kushiriki moja kwa moja lakini ilibidi tuombe Msaada wa ziada baada ya kufanya tathimini tukaona tunahitaji magari ya aina hiyo”

“Pamoja na misaada iliyokuja na shughuli za uokozi kwa sababu wanajeshi wa jeshi la Wananchi wa Tanzania pamoja na vyombo vingine vya Dola wanashiriki katika uokoaji Sasa hii itatuongezea nguvu na tutakwenda vizuri zaidi”

Hatahivyo Kunenge alipongeza Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kulinda mipaka ya taifa letu na wakati wa amani kuendelea kuhudumia jamii ya watanzania.

“Kama tunavyofahamu jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ tangu kuundwa kwake linalinda mipaka ya nchi na wakati wa amani linafanya shughuli za kijamii na shughuli hizi za huduma ikiwa ni pamoja na uokoaji pamoja na kupeleka chakula maeneo yanayohusika”

“Kwa hiyo nishukuru hata kwa jeshi letu kwakuwa kufanya hivyo hata wananchi wanaona ni jeshi lao hivyo nishukuru sana kwaajili ya waliofanya maamuzi ya kutuletea Msaada huu” alisema Kunenge

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!