Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu akimwagilia maji kwenye mti alio uotesha jana katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ikiwa ni kampeni ya kuhifadhi uoto wa asili katika mlima huo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu akiotesha mti katika eneo la Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, lililopo Kijiji cha Mengeni Kitasha Wilaya ya Rombo, zoezi la upapandaji miti linafadhiliwa na Tigo wakishirikiana na WWF.
Mgeni rasmi kwenye Kampeni ya Tigo Green for Kili , Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mengeni Kitasha Wilaya ya Rombo, kwenye kampeni ya kuotesha miti katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, Mei 21 , 2024.
Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Raimond Mwangwala, akimwagilia maji kwenye mti alio uotesha Mei, 21 , 2024 katika kijiji cha Mengeni Kitasha Wilaya ya Rombo kwajili ya kutunza mazingira kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.