Home Kitaifa RC KATAVI AZISHUKIA KAMPUNI ZA KUSAMBAZA MBOLEA KATAVI

RC KATAVI AZISHUKIA KAMPUNI ZA KUSAMBAZA MBOLEA KATAVI

📌📌 AZITAKA KUACHA VISINGIZIO KUSAMBAZA MBOLEA KWA WANANCHI BADALA YA KUFICHA.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko ameziagiza kampuni za usambazaji mbolea ya ruzuku mkoani humo kuhakikisha mbolea inawafikia mawakala badala ya kuificha kwenye maghala yao.

Mrindoko ametoa maagizo hayo Januari 3, 2023 baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika baadhi ya maghala ya makampuni hayo yaliyo Manispaa ya Mpanda na kushuhudia shehena kubwa ya mbolea ikiwa imerundikwa badala ya kuwa kwa mawakala.

Akiwa katika ghala la Kampuni ya mbolea ya Yara, RC Mrindoko ameambiwa kuwa sababu inayofanya mbolea kutokwenda kwa mawakala ni kutokana na serikali kufanya malipo hivyo mawakala kuzidiwa na madeni.

Kufuatia maelezo hayo RC Mrindoko akaagiza wasimamizi wa kampuni hiyo na kampuni zingine zilizoidhinishwa kusambaza mbolea mkoani humo kuhakikisha mbolea inawafikia wakulima vinginevyo ataamuru jeshi kuingia kwenye maghala hayo kusambaza mbolea wenyewe.

Katika hatua nyingine RC Mrindoko amewataka mawakala wa mbolea ya Ruzuku mkoani humo kuwafikia wakulima katika maeneo waliyojiandikishia ili kuwapunguzia adha ya kufuata mbolea mjini Mpanda.
Amewaagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha wanasimamia zoezi hilo ili adhma ya serikali kuweka ruzuku kwenye mbolea iweze kuonekana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!