Home Michezo RC KANALI MTAMBI ATOA RUHUSA KWA VIONGOZI NA WANANCHI KWENDA TABORA KUISHANGILIA...

RC KANALI MTAMBI ATOA RUHUSA KWA VIONGOZI NA WANANCHI KWENDA TABORA KUISHANGILIA BIASHARA UNITED

Na Shomari Binda- Bunda

MKUU wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi ametoa ruhusa kwa viongozi na wananchi kwenda mkoani Tabora kuishangilia timu ya Biashara United.

Biashara United kesho jumapili inashuka kwenye dimba la Ally Hassan Mwinyi Tabora kuikabili timu ya Tabora United kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa play off kuelekea ligi kuu.

Akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga ukatili dhidi ya wazee yaliyofanyika kitaifa leo juni 15 mjini Bunda amesema baada ya maadhimisho hayo tukio linalofuata ni kwenda kuishangilia Biashara United mkoani Tabora.

Amesema ruhusa hiyo anaitoa kwa wakuu wa wilaya wote, makatibu tawala na wakurugenzi wawape fursa madiwani na wananchi waende kuongeza nguvu Tabora.

Kanali Mtambi amesema mchezo huo ni muhimu katika kuhakikisha ushindi unapatikana na kurejea ligi kuu msimu ujao.

Amesema timu ya Biashara United ni nzuri na kilichobaki inahitaji sapoti ya mashabiki kwenye mchezo huo.

“Tumemaliza tukio hili la maadhimisho ya kupinga ukatili dhidi ya wazee na maelekezo yametolewa sasa ni tukio la kwenda Tabora”

“Natoa ruhusa kwa wakuu wa wilaya baada ya hapa tuanze safari na wakurugenzi muwawezeshe madiwani waende Tabora kutia nguvu” amesema.

Mkuu huyo wa mkoa amewaomba wazee kuiombea dua timu hiyo ili iweze kufanya vizuri kwenye mchezo huo na kufikia lengo.

Kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliofanyika juni 12 kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Karume Musoma timu ya Biashara United ilishinda bao 1-0

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!