Home Kitaifa RC CHALAMILA: UWEKEZAJI WA MIRADI MIKUBWA YA KIMKAKATI KAGERA KUKWAMUA MKOA KUTOKA...

RC CHALAMILA: UWEKEZAJI WA MIRADI MIKUBWA YA KIMKAKATI KAGERA KUKWAMUA MKOA KUTOKA KWENYE UMASIKINI

Theophilida FeFelicia, Kagera

Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe Albert Chalamila amesema kuwa juhudi mbalimbali zinazofanya na Serikali chini ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassani katika kuileta miradi kadhaa ya uwekezaji kimkakati inatarajiwa kuwa miongoni mwa kasi kubwa ya kuleta mageuzi zaidi kiuchumi mkoni Kagera.

Akiitaja baadhi ya miradi hiyo kwenye kikao cha baraza la wafanyabiashara Mkoa kilichofanyika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manispaa ya Bukoba amesema kuwa mmoja wa mradi mkubwa ni ule wa ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba wenye thamani ya Dola Bilioni moja utakaojengwa kata ya Rubafu Halmashauri ya Bukoba mwambao na ziwa Victoria.

“Hivi tunavyozungumza tayari watalaamu kutoka wizara mbalimbali wameishafika hapa Kagera wameenda kule Rubafu ile Rubafu yote itakuwa na uwekezaji usiopungua Dola Bilioni moja sasa watu wanadhani ni utani utani tuu, mradi huu mpaka kufikia hatua yakuanza kufanya kazi kunatakiwa vibali( 21) navyozungumza nanyi muda huu vimebakia vibali viwili tuu hivyo kwa mtu yeyote atakayetaka kuwekeza katika eneo hilo leseni itakuwa ni moja pekee niwahakikishie mradi huu ukianza utekelezaji utategua mtego wa umasikini wa Mkoa wetu” Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila akiwaeleza bayana wafanya biashara walioshiriki katika kikao hicho.

Amesema kuwa katika mradi huo kutajengwa nyumba zaidi ya (1000) za wa fanyakazi nawa tu wengine huku kukijengwa chuo cha utafiti wa mbegu za samaki na vyakula vya samaki chini ya chuo kikuu cha Nelisoni Mandela kitakacho jengwa kata ya Kahororo Manispaa ya Bukoba.

Miradi mingine ameitaja kuwa ni ujenzi wa tawi la chuo kikuu cha Dar es salaam ambacho ujenzi wake utaanza muda si mrefu baada yakukamilisha kwa taratibu chache zilizobakia sambamba na ujio wa bomba la mafuta ghafi litakalotokea nchi ya Uganda.

Mbali na hayo ameigusia baadhi ya miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa na itakayotekekezwa na Serikali ikiwemo ya ukarabati wa bandari ya Bukoba na Kemondo, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha rami hususani barabara ya Bugene Karagwe kwenda Kasulo Ngara ambapo ujenzi umeishaanza kwa kilomita ( 60) kati ya kilomita (120) za barabara hiyo.

Hata hivyo amewahakikishia wafanyabiashara na wawezaji kwa ujumla kuwa jitihada thabiti zinafanyika ili kuhakikisha Mkoa wa Kagera unafunguka kiuchumi na kuongeza kiwango cha mzunguko wa kifedha kuliko hali ilivyo kwa sasa.

Kaist Kabenga kutoka baraza la wafanya biashara taifa awali amempongeza Mkuu wa Mkoa Chalamila kwa namna anavyojitahidi kupambana ili kuupandisha kiuchumi Mkoa kutoka hapo ulipo

“Ili kuweza kufanikisha hili la kuusaidia mkoa tujipangeni kuzitiza upya taratibu za mifumo isizo rafiki tulizojiwekea katika uwekezaji nimefulahi ukisema katika uwekezaji wa mradi wa samaki mmetakiwa kuwa na vibali ( 21) hapo ni kwaupande wetu Serikali nisahihi kabisa make ni taratibu tulizojiwekea sasa tuashumu kwa wenzetu kutoka nje ya nchi ninani atakubali kufanya hiyo biashara? sana sana watatusikiliza mwisho watapanda ndege na kuondoka wakituacha na milolongo yetu hiyo na vyoona hapa kuna haja ya kuvilekebisha vitu hivi ili mazingira ya uwekezaji yawe rafiki kwa wote si kwa wananchi si kwa wageni Mama ameishaifungua nchi kazi ni kwetu” Kaist Kabenga akieleza.

Pia suala jingine amezungumzia umuhimu wa Mkoa Kagera kuona jinsi agani ya kuvipunguza vikwazo vilivyopo ndani ya uwezo wao ambavyo ni mzigo hususani vile vyenye kuzibana sana biashara za maeneo ya mipaka ya nchi za Afrika Mashariki kwakufanya hivyo itakuwa ni njia sahihi ya kulahisisha na kuwapa motisha wananchi wanaoishi mipakani kufanya biashara kwa kiwango cha juu na wenzao wa nchi hizo ambazo ni Uganda, Rwanda, Burundi, Congo na Kenya.

Kwa upenda wake Katibu tawala wa mkoa Kagera Mhe Toba Nguvula amewasihi wananchi na wafanya biashara kuendelea kuzichangamkia fursa zinazokuja hali itakayowawezesha kuongeza kipato ambapo amezishauri Halmashauri kuchangamkia fursa za kutenga maeneo ya kujenga maghara ya mizigo maeneo ya mipakani.

Nao baadhi ya wafanya biashara na wawekezaji akiwemo Bakuza Ahamada naye Leonard Fausten ambao ni wafanya biashara wa mazao ya kahawa na mchele wameshuri ifanyike mikakati ya kujenga magodauni makubwa yakuweka mizigo hasa eneo la Kyaka Misenyi na maeneo ya Kyerwa katika mpaka wa Uganda kwa malengo yakuongeza mzunguko wa fedha na ajira kwa watanzania na wageni kwa maana kwamba wafanya biashara wanaokwenda kufuata mizingo mikoa ya nje hawatafanya hivyo badala yake watachukua mizigo maeneo hayo.

Odetha Pasco ni mfanyabishara kutoka Rusumo Ngara karibu na mpaka wa nchi ya Rwanda yeye ameelezea changamoto zinazo wakabili katika biashara zao wawapo nchini ya Rwanda moja ni kutokuzifahamu lugha za kifaransa na kinyarwanda changamoto ambayo huwasababishia kuibiwa fedha za mauzo nyakati za kubadilishiwa pesa ameiomba Serikali kuona haja yakuweka watu wanaozifahamu lugha za kigeni katika mipaka ili kuwasaidia wananchi kuelewa matumizi ya lugha hizo hiyo itawasaidia kuendesha biashara zao bila ya bughudha za kuibiwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!