Home Kitaifa RC CHALAMILA ATOA NENO KWA VIONGOZI WA DINI KUKEMEA MMOMONYOKO WA MAADILI

RC CHALAMILA ATOA NENO KWA VIONGOZI WA DINI KUKEMEA MMOMONYOKO WA MAADILI

Na Magrethy Katengu

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamala amewataka viongozi wa Dini kusaidia kukemea tatizo la Mmomonyoko wa maadali ikiwemo ubakaji, usagaji, wizi, ushoga vitendo ambavyo vinaathiri jamii na kizazi kijacho.

Wito huo ameutoa Jijini Dar es salaam katika Baraza la Amani la Mkoa wa Dar es salaam lililowajumuisha viongozi wa Dini mbalimbali ambapo amesema Mna kulingana na Mamlaka mliyo nayo mna Wadhifa mkubwa kupitia hotuba na Mawaidha mnayotoa katika nyumba za ibada kuweza kusaidia tatizo la Mmomonyoko wa maadili likapungua na kusaidia kizazi kijacho

Biblia takatifu na Quraan tukufu ni vitabu vya Mwenyezi Mungu alivyowatumia Manabii na Mitume kuandika maandiko ambayo akisoma mwanadamu kulingana na falsafa mbalimbali zenye kusisitiza kuishi maisha matakatifu na kumwamini Mungu hivyo Mimi naamini wengi wamebadika kupitia vitabu hivyo” amesema Chalamila

Chalamila Kwa siku za hivi karibuni tabia za kishetani zimekuwa zikiibuka kwa kasi miongoni mwa jamii na Shetani amekuwa akitumia mbinu hizo ili ili kuiangusha jamii hivyo ni vyema kila mwanadamu kuwa makini siyo kila jambo geni ni lakuiga ni mbinu za ibilisi kuleta madhara katika jamii yetu.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Sheikh Walidi Kawambwa Nchi ya Tanzania Seikali haina Dini ila Wananchi wake wana Dini hivyo amemshukuru Mkuu wa Mkoa huyo kuwaita kwa pamoja na kuzungumza naye na kuweka Baraka katika uongozi wake.
Hapo Nyuma tumekuwa na makundi mbalimbali ikumbukwe kuwa nchi hii Haina dini ila raia wake wana dini” . Alisema shelk Walidi kawambwa .

Aidha imesisitizwa kuwa kila mtu anapaswa kuwa balozi kwa kusaidiana kulinda amani iliyopo kwani ni tunu kubwa iliyoachwa na Tanzania ni nchi ya makimbilio kwa walio wengi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!