Na Theophilida Felician Kagera.
Wakulima katika Kijiji cha Ibaraizibo kata Karabagaine Halmashauri ya Bukoba Mkoani Kagera wamekilalamikia kiwanda cha chai Kagera TEA LTD kwakushidwa kutimiza wajibu wa kuwalipa madai yao ya manunuzi ya mazao ya chai Sh Milioni (65)
Wakulima hao wametoa malalamiko yao mbele ya Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe Albert Chalamila akiwa ametembelea kiwanda hicho leo hii tarehe 6 January mwaka huu.

Baadhi ya wakulima ambao wameonekana kusononeshwa na kero hiyo akiwemo Mzee Nestor Rugakingira, Mzee Yahaya Salumu, Bi Adentina Nestor pamoja naye Theophili Laurent kwapamoja wameeleza kuwa madai ya pesa zao hizo ni yatangu mnamo mwaka wa (2020)
“Mhe Mkuu wa Mkoa toka mwaka wa (2020) hadi sasa hatujapata hata senti tumehangaika sana na mwekezaji huyu ili atupatie haki zetu lakini bado kuna kipindi alitulipa baada ya kufikishwa mahakamani tukuombe Mhe tusaidie mtu huyu amekuwa ni tatizo kwetu kwa muda murefu abadilishwe aje mwekezaji mwingine hapa tulipo tumeishajipanga kufunga safari yakwenda kwa Mhe Rais tena tunakuomba mchango wako wa laki moja yakutuwezesha kutusaidia kwenda kuonana na Mkuu wa nchi hii hatukufichi tunakueleza wazi wazi tumechoka na wizi wa Kampuni hii” wamesikika wakipaza sauti zao wakulima hao.
Wameendelea kumweleza Mkuu wa Mkoa kwamba kutokana na kukwama kwa pesa zao hizo imewapelekea wengi wao kushindwa kutimiza malengo ya majukumu yao hususani kipindi hiki cha maandalizi ya kuwapeleka shule watoto pamoja na mahitaji mengine muhimu katika familia zao.
Wameiomba Serikali kuchukua hatua madhubuti zitakazosaidia kupata malipo yao hao.
Nao wafanyakazi akiwemo Resipicus Alfred pamoja naye Antius Paulo wemesema kuwa wanakidai kiwada hicho malimbikizo ya madeni mbalimbali tangu mwaka wa (2019) mpaka sasa hawajalipwa hata mishahara yao.
Meneja wa kiwanda Salumu Joseph akimwakilisha mmilikiwa wa kiwanda halisi amekili kuwepo kwa changamoto kadhaa ikiwemo ya madai hayo ya Sh Milioni (65 )ya wakulima pia na madai mbalimbali ya wafanyakazi ambapo amezitaja sababu mbalimbali zilizopelekea hali hiyo hasa kushuka kwa bei ya chai, masoko ya nje ya chai ambayo ni Mombasa Kenya na Rwanda kufungwa kipindi cha mlipuko wa ugonjwa wa Corona na nyinginezo.

“Mhe Mkuu wa Mkoa kutokana na changamoto hizo za madeni baadhi ya wafanyakazi wametukimbia hivyo nguvu kazi ya uzalishaji imepungua kwa sasa kiwango cha uzalishaji wa kiwanda ni chini ya 25% tofauti na hapo nyuma, hivyo licha ya ugumu huu tunaendelea kufanya kila liwezekanalo ili tulipe madeni haya yote kwa wakulima na wafanyakazi kwaupande wa wakulima mwezi Novemba mwaka jana tulipanga kuwa ifikapo mwezi Desemba tuweze kuwalipa lakini hatukuweza kufanya hivyo kwani tulikuwa hatujaikamilisha pesa hiyo ila ndani yakipindi kifupi tutawalipa” amesema Meneja Salumu Joseph.
Mkuwa Mkoa Chalamila hakuweza kutoa majibu ya moja kwa moja kutokana na kutokumkuta mmiliki halisi wa kiwanda hicho baada yakupewa taarifa na meneja kuwa yuko nje ya nchi Jambo lililomplekea kumtaka ajitokeze ndani ya kipindi cha wiki moja.
“Ndugu zanguni wananchi siwezi kuzungumza na mwakilishi aje hapa mmiliki wa kiwanda hiki tuzungumze ni namna gani ya kutatua matatizo haya, niwasihi sana tuzidi kuwa watulivu wakati tukiendelea kushughulikia masuala haya lazima yapate ufumbuzi ili kila mmoja apate stahiki zake make yapo mambo mengi ya kushaurina juu ya hii” Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila akiwaeleza wakulima hao na wafanyakazi.

