Ashrack Miraji Same Kilimanjaro
Kuelekea Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Kilimanajaro Aprili 02,2024 RC Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu amewaomba viongozi na madereva wa bajaji ushirikiano katika Kutoa huduma ya usafiri iliyobora kwa wagen wanaotarajiwa kufika Mkoani hapa.
Amesema hayo leo Machi 19,2024 wakati wa kubandika vipeperushi (stiker) zenye ujumbe wa Uzinduzi wa Mwenge kwenye bajaji katika kituo cha KCMC na kukabidhi viongozi wa Bajaji vipeperushi kwa ajili ya kusambaza kwenye bajaji zote hapa Mkoani.
Aidha, Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Tixon Nzunda amesema Mkoa umepewa heshima ya kuzindua Mwenge wa Uhuru mwaka huu hii ni kutokana na Mwenge wa Uhuru kutimiza miaka 60 tangu kupandishwa kilele cha Mlima Kilimanjaro na kuanza rasmi kwa mbio,vile vile Taifa kutimiza miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar pamoja na miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na miaka 25 ya kumbukizi ya Muasisi wa Taifa letu baba wa Taifa Mwl. Julias Kambarage Nyerere tangu atutoke.