Na. Magrethy Katengu
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amosi Makala amewataka Viongozi wa Halmashauri kusimamia Majukumu ya vizuri na kugawa raslimali zote Kwa kuzingatia Idadi ya watu wanaowaongoza.
Agizo Hilo amelitoa jana Jijini Dar es salaam wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Sensa ya 2022 yalioyoshirikisha Wakuu wa Wilaya,Wenyeviti wa serikali za Mitaa ambapo amesema Mkoa wa Dar es salaam takwimu halisi ya Idadi ya watu imepatikana hivyo huduma za Kijamii zitatolewa kulingana na takwimu iliyotolewa
“Idadi ya watu nchini mwaka 2012 ilikuwa Million nne laki tatu mia sita sitini na nne elfu miatano arobaini na Moja na Sensa iliyofanyika mwaka 2022 Idadi ilikuwa milioni tano laki tatu themanini na tatu elfu miasaba ishirini na nane matokeo haya yanasaidia kutoa huduma kwa Jamii kulingana na idadi yao”amesema Makala.
Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi Sensa na Takwimu ya Makazi ya Watu Ruth Minja amesema Serikali ilitoa fedha nyingi kuhakikisha zoezi la kuhesabu watu linakwenda kama ilivyokusudiwa hivyo takwimu hiyo itasaidia hata watafiti wanapofanya shughuli za wasihangaike sana au kutumia gharama kubwa.
Naye Kaimu Mwenyekiti wa Wenyeviti Mkoa wa Dar es salaam na pia ni Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Wilaya ya Kinondoni Razalous Anosisye Kiposa amewasa Wenyeviti kufuatilia takwimu za kila kata wanazoziongoza wajue wanaongoza watu wa ngapi Ili kuwapa huduma za Kijamii kulingana na idadi yao.