Home Michezo RAIS WA TFF APEWA SAA 72 KUOMBA RADHI.

RAIS WA TFF APEWA SAA 72 KUOMBA RADHI.

Umoja wa Wazee wa Timu ya Yanga Mkoani Dodoma watoa Saa 72 kwa Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Bwana Wallace Karia kuomba radhi kufuatilia kauli aliyoitoa kuhusu timu yao.

Kauli hiyo ya Wazee imetolewa leo Machi 18,2025 jijini Dodoma wakizungumza na Waandishi wa habari na Mzee Abdalah Mtosa kwa niaba ya wazee wengine huku akisisitiza hawaoni sababu ya kurudia mchezo ambao tayari ulipangwa kisheria na kuahirishwa bila utaratibu siku ya Machi 8,2025

Mzee Mtosa ameeleza kuwa siku ambayo ilikuwa halali kwa mchezo huo kuchezwa tayari imepita na ilikuwa inatosha kabisa kuwakutanisha watani kwani maandalizi yote yalikuwa yameshakamilika.

Nimepokea kwa masikitiko makubwa sana Kwa kuahirishwa kwa mchezo wa Machi 8 mwaka huu, kwahiyo na sisi hatuna imani na karia kwani tunajua wazi hana mapenzi ya dhati na yanga
hivyo niwaombe viongozi wa juu kutokuruhusu mechi kufanyika tena Kwa wakati mwingine kama ni faini tuko tayari kulipa lakini sio kurudia mechi na simba
“. amesema Mtosa

Kwa upande wake Mzee Bodar Awadhi amesema mechi kuahirishwa imefanya kutokea mkanganyiko na sintofahamu kwa mashabiki wa soka na hivyo kundi kubwa halitaki tena hiyo mechi.

Sisi msimamo wetu ni kutokurudia mechi kwanza RAIS wa TFF ametudhalilisha wanayanga na kama ameshindwa mpira arudi kwenye taaluma yake kwani tunaijua

Kwa upande wake Mratibu wa yanga Dodoma Elisha Ngwando amesema Karia aombe Radhi kwa Wanachama wa Yanga na wanamichezo kwa alichokifanya na kauli aliyoitoa.

Watu wametumia gharama kubwa wengine wamelipia matangazo kwa ajili ya mechi hiyo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!