Home Kitaifa RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AMETEMBELEA...

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AMETEMBELEA KIWANDA CHA TANGANYIKA WATTLE COMPANY LIMITED

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Leo tarehe 10 Agosti, 2022 ametembelea kiwanda Cha Tanganyika Wattle Company Limited (TANWAT) na kuzungumza na wananchi wa Mkoa wa Njombe.

Kiwanda Cha TANWAT Kinajihusisha na uzalishaji wa nguzo za umeme, Dawa ya kutibu Ngozi (Tanin), plywood, mbao na umeme Megawatt 2 ambapo 0.7 megawatt wanatumia wenyewe na Megawatt 1.3 wanawauzia Tanesco,

Kiwanda hiki Cha Tanganyika Wattle Company Limited kimeajiri wafanyakazi wakudumu 1300.

Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amezungumza na wananchi wa Mkoa wa Njombe na kuwataka kuendeleza ushirikiano kwa uongozi wa Mkoa na Wilaya ili mambo yaendelee kuwa mazuri zaidi.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amewashukuru viongozi wote kwa kazi nzuri ya kukusanya mapato, kuna uwezekano wa kukusanya zaidi, hivyo kuwataka kuongeza juhudi ya kukusanya mapato ili Serikali anayoiongoza iendelee kutekeleza miradi ya maendeleo.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Kwa Sasa tuko katika maandalizi ya awamu ya pili ya filamu ya Royal tour itakayoitwa “The hidden Tanzania” ikiwa na lengo la kutangaza maeneo mengine yenye vivutio vya utalii vilivyomo nchini Tanzania.

Mhe. Rais Samia ameongeza Kwa kusisitiza wananchi kuhesabiwa katika Sensa ya Watu na Makazi ili wananchi kupata huduma kwa idadi ya watu waliopo.

Aidha, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa mradi wa Liganga na Mchuchuma ni mradi wa kimkakati na imegundulika kuwa Kuna aliyekuwa akijiita Muwekezaji sio Mwekezaji hivyo tutamuondoa.

Mhe. Dkt. Kijaji amesisitiza kuwa Serikali inahitaji Mwekezaji makini na mahiri atakayetunufaisha Watanzania.

Mhe. Dkt. Kijaji amemaliza Kwa kusema kuwa tayari tumepata Mwekezaji katika Mradi wa Maganga Matitu ambapo mkataba tutakaoingia kwenye mradi huu ni mkataba huru ambao Mwekezaji akishindwa ataondolewa.
Suala la kupanda kwa bidhaa za sabuni, hii imetokana na nchi ya Indonesia kuweka zuio la kuuza nje (export ban) malighafi hiyo ya kutengeza sabuni na kwa maana hiyo ikapelekea kupanda kwa bei. Hata hivyo tumeongea na wenye viwanda na kuahidi kuwa bei itapungua kwa sababu kwa sasa Indonesia imeshafungua soko (removing ban), na sasa wameahidi kuwa ifikapo mwezi Septemba bei inaweza kupungua.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!