Home Kitaifa RAIS SAMIA MGENI RASMI SIKU YA MASHUJAA –MAJALIWA ASEMA AMERIDHISHWA NA MAANDALIZI.

RAIS SAMIA MGENI RASMI SIKU YA MASHUJAA –MAJALIWA ASEMA AMERIDHISHWA NA MAANDALIZI.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan atakuwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya siku ya Mashujaa, yatakayofanyika kitaifa Julai 25, 2022 Mkoani Dodoma.

Amesema hayo leo (Jumamosi, Julai 23, 2022), baada ya kukagua maandalizi ya maadhimisho hayo, katika viwanja vya Mashujaa Mkoani Dodoma. Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na maandilizi yaliyofanywa na kamati ya maadhimisho kitaifa kwa kushirikiana na vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akikagua maandalizi ya kuelekea siku ya Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mashujaa katika Uwanja wa Mnara wa Mashujaa Jijini Dodoma tarehe 23 Julai, 2022.

“Sherehe hii itafanyika kitaifa mkoani Dodoma na itaongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Viongozi wastaafu na viongozi wengine wa kitaifa.”

Waziri Mkuu amesema, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan aliridhia maadhimisho hayo yafanyike kitaifa mkoani Dodoma, lakini akaelekeza yafanyike nchi nzima kwa Wakuu wa Mikoa kuadhimisha siku hiyo kwa kwenda kwenye maeneo muhimu ya kumbukumbu kwenye mikoa yao.

Aidha, Waziri Mkuu amevipongeza vyombo vya habari kwa namna ambavyo vimekuwa vikishiriki katika kutoa hamasa kwa wananchi kushiriki katika matukio mbalimbali ya kitaifa na kwamba Serikali inathamini mchango huo.

“Serikali inawashukuru sana wananchi kwa namna ambavyo wanajitokeza katika matukio haya ya kitaifa na kujanza viwanja, tunaamini pia Julai 25 watajitokeza kwa wingi.”

(Mwisho)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!