Na. Mercy Maimu
Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa salamu za sikukuu za Krimasi na Mwapa Mpya huku akiwataka watumiaji wa barabara kuchukua tahadhari.
Rais Samia ametumia akaunti zake za kijamii za Twitter na Instagram kutoa ujumbe huo ikiwa ni siku na masaa machache yamebaki kabla ya Wakristo wa Tanzania kuungana na wenzao duniani kusherekea sikukuu hizo.
Ameandika ujumbe huo akiuambatanisha na picha ya barabara akisema,
“Panapo majaliwa, siku chache zijazo tutasherehekea sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.”
“Nawatakia nyote kheri katika sherehe hizi ili ziwe za furaha na zisizo na misiba inayoweza kuepukika,” ameandika Rais Samia na kuongeza
“Nawasihi wasafiri na madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuchukua tahadhari.”