
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka Wakurugenzi wa halmashauri, wakuu wa wilaya na viongozi wengine katika serikali za mitaa kutoa taarifa mapema kama wana mpango wa kugombea ubunge.
Msingi wa kauli ya Rais Samia ni kutaka nafasi zao zijazwe mapema na watu wenye sifa huku akiwaonya kutoshitukiza wakati wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, akisema watakaosema mapema ipo hatihati ya kukosa yote huku wale watakaotoa taarifa mapema ikiwa watashindwa ipo nafasi nyingine ya kuweza kurejeshwa tena serikalini

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumanne Machi 11, 2025 jijini Dodoma katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa 39 wa viongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (Alat) akisisitiza kuwa hakuna umuhimu wa mtu kwenda kwenye uchaguzi kwa kubahatisha bali uchaguzi ufanyike kukiwa na watu makini katika harakati hizo za uchaguzi.