Home Kitaifa RAIS SAMIA AMEFANYA UTEUZI WA VIONGOZI.

RAIS SAMIA AMEFANYA UTEUZI WA VIONGOZI.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Viongozi katika nafasi mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus leo  Aprili 12, 2024 imeeleza kuwa CPA Anthony Mzee Kasore ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA). Kabla ya uteuzi huu, CPA Kasore alikuwa akikaimu
nafasi hiyo.

Imeeleza kuwa Bw.Goodluck Antipas Shirima ameteuliwa kuwa Kamishna wa Petroli na Gesi, Wizara ya Nishati. Bw. Shirima ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Uhusiano Kampuni ya Mafuta ya Puma, Tanzania.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!