
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi, Dtk. Hussein Ali Mwinyi amewahimiza waumini wa dini ya kiislamu kuishi kwa kufata misingi ya dini pamoja na kufanya ibada.
Rais Mwinyi,ameyasema hayo leo katika mashindano ya Tajwiid Qur’an yaliofanyika katika masjid jamiu zenzibar mazizini wilaya ya mjini,yaliandaliwa na Tasisi ya Al Hikm Qur’an foundation.

Rais Mwinyi amesema kazi kubwa inayofanywa na masheikh na walimu wa dini kusomesha vijana na kuwapatia uwezo wa kuifadhi Qur’an inapaswa kuungwa mkono na kila mmoja.
Pia amewasihi waislamu kufata miongozo ya dini hiyo pamoja na kuzidisha bidii ya kusoma Qur’an na kuwasimamia watoto wao kuwa na mwenendo mzuri wakati wa mwezi wa Ramadhani.
Pia amewapongeza wadhamini wanaendelea kuyafadhili mashindano hayo kila mwaka na kuwaomba wengine wajitokeze kuunga mkono jitihada hizo.
