Home Kitaifa RAIS MWINYI AHIMIZA JAMII KUWA NA MAZINGIRA MAZURI YA FURSA KWA YATIMA

RAIS MWINYI AHIMIZA JAMII KUWA NA MAZINGIRA MAZURI YA FURSA KWA YATIMA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi ameeleza haja kwa jamii kujitahidi kuwajengea mazingira mazuri yatima yatakayowapa fursa na kuwaondolea huzuni na ukiwa wa kuondokewa na wazazi wao.

Alhaj Dk. Mwinyi alihimiza juu ya umuhimu wa wazazi kushirikiana na kuongeza bidii katika malezi ya watoto na kuitaka jamii kutekeleza wajibu wake; kwani bila ya shaka wakiwalea watoto vizuri, itakuwa rahisi kufahamu umuhimu wa kuishi na wenzao walio yatima.

Alhaj Dk. Mwinyi ameeleza hayo leo katika dua ya Kitaifa pamoja na dhifa ya chakula cha mchana kwa ajili ya watoto yatima, hafla iliyoandaliwa na Jumuiya ya Nuru Foundation kwa kushirikiana na Jumuiya mbali mbali pamoja na Ofisi ya Mufti wa Zanzibar, iliyofanyika katika uwanja vya Mao Tse Dong, Zanzibar.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!