Home Kitaifa RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN KUFANYA ZIARA NCHINI KOREA KWA SIKU 6

RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN KUFANYA ZIARA NCHINI KOREA KWA SIKU 6

Na Magrethy Katengu— Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya Ziara ya kikazi Nchini korea siku sita kuanzia Mei 30, 2024.

Akitoa taarifa hiyo leo Jijini Dar es salaam Mei 29, 2024 Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Januari Makamba amesema ziara hiyo italeta tija kwa Tanzania kwani Serikali itaingia Mkataba wa wa Msaada wa mkopo nafuu wa Dola za Kimerekani 2.5 bilion sawa na shilingi 5.2 trilion kutoka serikali ya Korea fedha hizo zikienda katika sekta mablimbali ikiwemo Elimu, Afya na miundombinu .

“Makubaliano haya ni mapya ya Ushirikiano wa maendeleo kati ya Serikali ya Tanzania na Korea na Mkataba huu ni mkubwa kati ya saba itakayoingia Juni 2, 2024 kati ya Taifa hili na nchi hiyoo” amesema Waziri

Sanjari na hayo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan atafanya mazungumzo na kusaini mikataba saba ya ushirikiano kati ya Tanzania na Korea na Hati ya makubaliano kati ya Taasisi ya Madini Tanzania. GST na Taasisi ya miamba nchini korea ushirikiano kuhusu utafiti, uchoraji ramani, rasilimali na uchoraji wa maabara.

Pia Mkataba wa pili ambao unaenda kusainiwa kati ya Rais Samia na Rais wa Korea ni ushirikiano wa uchumi huku mkataba wa tatu ukihusu kwenda kutambua vyeti vya Mabaharia pia wataweza kusaini Tamko la pamoja kuhusu siasa na makubaliano ya hati ya Madini, Viwanda na biashara.

Aidha Waziri Makamba ameongeza kuwa kuhusu madini kwenye mkakati watasaini mkataba katika kuwezesha kuchambua na kufanya Mkakati na shirika la madini Tanzania STAMICO na shirika la ukarabati wa madini nchini Korea.

Hata hivyo Mkataba mwingine ni Msaada wa fedha kutoka benki ya Exim nchini Korea na serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambao unaenda kupelekea nchi yetu kupata msaada na mikopo nafuu Takribani dola mbili nanusu vilevile wataenda kushirikiana na chuo kikuu kutoka nchini korea katika kuendeleza huduma za usafiri wa anga nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!