Home Kitaifa RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSANI ANATARAJIWA KUFANYA ZIARA NCHINI INDIA

RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSANI ANATARAJIWA KUFANYA ZIARA NCHINI INDIA

Na Magrethy Katengu

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani anatarajiwa kufanya ziara ya Kitaifa ncgi India Octoba 8hadi 11 Mwaka huu akiambatana na Wafanyabiashara kuangalia fursa za kibiashara na Uwekezaji kiuchumi.

Akitoa taarifa hiyo kwa Waandishi wa habari Leo Jijini Dar es salaam Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Januari Makamba ambapo amesema Rais atawasili nchini India /Octoba 8 na siku inayofuata ya tarehe 9 atapokelewa na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa India.

Waziri January Makamba amesema kuwa Madhumuni ya ziara hiyo ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kukukuza ushirikiano wa kidiplomasia yakiuchumi baina ya Tanzania na india katika sekta za ikiwemo Ulinzi, Maji, kilimo, Afya, Biashara na uwekezaji.

“Moja ya Mashirikiano yetu na nchi ya india ni katiks sekta ya afya kwani imefanikiwa sana kwa sekta hiyo hivyo kupitia ziara hiyo tutaanzisha taasisi ya upandikizaji Figo pia kiwanda cha kutengeneza chanjo za binadamu na wanyama, na Kuboresha utaalamu katika sekta ya ikiwemo , upatikanaji wa dawa katika uboera na weledi” amesema Waziri Makamba.

Waziri Makamba abainisha kuwa katika sekta ya kilimo ziara italeta fursa ya kukuza Masoko ya Mazao ya kilimo ikiwemo Mbaaz korosho na kuhakikisha soko hilo linaendelea kuwepo na kuongezeka pia kuanzisha konga i ya viwanda ndani ya Tanzania

Pia amesema kwa kuwa nchi ya India imeendelea katika sekta ya maji hivyo italeta uanzishwaji wa karakana utengenezaji wa vyombo vya Usafiri Majini kwani Tanzania kuna Mradi wa Maji wa ziwa Victoria bahari .

“Mikataba 15 ipi katika mazungumzo yatakapofikia muafaka itasainiwa kati ya Tanzania na india kuweka ushirikiano katika kutekeleza Diplomasia yauchumi kutafuta masoko na kuimarisha uwekezaji” amesema Waziri

Aidha Matuki atakayofanya Rais Dkt Samia Suluhu Hassani ni ikiwemo kwenda kuweka shahada la maua katika Kaburi la Mtu aliyekuwa mashuhuri nchini India Indira Ganzi pia atafanya mazungumzo ya faragha na Waziri Mkuu wa India atafanya mkutano na waandishi wa habari Kisha kukutana na wafanyabiashara waku wa katika kongamano.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!