Home Kitaifa RAIS DKT SAMIA AWAKUMBUKA WAKAZI WA NJOMBE KWA REA KUSAMBAZA MITUNGI YA...

RAIS DKT SAMIA AWAKUMBUKA WAKAZI WA NJOMBE KWA REA KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI YA KILO SITA.

*Mitungi ya gesi 13,020 kusambazwa mkoani Njombe

*Kila wilaya kupatiwa mitungi ya gesi 3,255

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeingia mkataba na mtoa huduma kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited ambaye atahudumia wilaya zilizopo ndani ya Mkoa wa Njombe kwa kuuza kwa bei ya ruzuku mitungi ya gesi ya kilo sita pamoja na vifaa vyake katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji.

Hayo yamebainishwa leo Januari 4, 2025 mkoani Njombe na Mhandisi wa miradi wa REA, David Malima wakati wa uzinduzi rasmi wa mradi wa ugawaji mitungi ya gesi ya kilo sita Kata ya Tandala, Wilaya ya Makete mkoani Njombe.

Mha. Malima amesema kuwa mitungi ya gesi 13,020 itakayosambazwa mkoani Njombe itachochea kwa kiasi kikubwa matumizi ya nishati safi na salama.

“Lengo la mradi ni kukuza, kuchochea, kuwezesha na kuboresha upatikanaji wa huduma za nishati safi ya kupikia ili kupunguza ukataji wa miti ambapo takribani hekta 400,000 hukatwa kila mwaka, ” Amesisitiza Mha. Malima.

Mha. Malima amesema, Serikali kupitia REA imetenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ikiwemo gesi (LPG) katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa mji na katika mkoa huo kiasi cha shilingi milioni 253.89 kimetengwa kutekeleza mradi huo.

Amezitaja wilaya zitakazonufaika kuwa ni pamoja na Wilaya ya Makete, Ludewa, Njombe na Wanging’ombe.

Kwa upande wake, Mtendaji wa kata ya Tandala , Bw. Maximillian Msigwa ameipongeza REA kwa kuja na mradi huo na kuiomba iwe endelevu ili iweze kuwasambazia wananchi wengi nishati hiyo muhimu Na kuchochea ustawi wa maisha ya wananchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!