Home Kitaifa RAIS DKT. SAMIA AMEWASILI ARUSHA KUSHIRIKI KUMBUKIZI YA SOKOINE

RAIS DKT. SAMIA AMEWASILI ARUSHA KUSHIRIKI KUMBUKIZI YA SOKOINE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili katika uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro KIA,tayari kwaajili ya kuelekea Wilayani Monduli Mkoani Arusha kwenye Kumbukumbu ya miaka 40 ya kifo cha Hayati Edward Moringe Sokoine, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mh.Rais Samia Suluhu Hassan amepokelewa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mh.Paul Christian Makonda na Mh. Nurdin Babu, Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.

Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuungana na Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na viongozi wengine wa serikali kwenye kumbukizi hiyo inayofanyika nyumbani kwa Hayati Sokoine, kijijini Enguiki wilayani Monduli.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!