Home Kitaifa RAIS DKT. MWINYI: SERIKALI KUTEKELEZA MIPANGO YA KUWASAIDIA VIJANA NA WANAWAKE...

RAIS DKT. MWINYI: SERIKALI KUTEKELEZA MIPANGO YA KUWASAIDIA VIJANA NA WANAWAKE KWA KILIMO BIASHARA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ya Tanzania pamoja na washirika wa maendeleo kwa pamoja wameandaa mikakati shirikishi na kutekeleza mipango mbalimbali ya kusaidia vijana na wanawake kujishughulisha na kilimo biashara.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 07 Septemba 2023 akizungumza katika mkutano unaoendelea wa Jukwaa la mifumo ya chakula Afrika unaofanyika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Aidha , Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa ushirikishwaji wa vijana na wanawake katika kilimo na uvuvi unatoa fursa nyingi katika kuendeleza uchumi unaotegemea kilimo vijijini.

Vilevile, Rais Dkt. Mwinyi amesema mkutano huu unalenga kuhamasisha washirika wa maendeleo kusaidia mpango wa BBT wa Tanzania kwa ajili ya kuongeza ajira kwa vijana na wanawake katika mifumo ya chakula.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!