Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amekipongeza Chuo cha Maji na kumtaka Mkuu wa Chuo hiko Dkt.Adam Karia kuendelea kutoa huduma zake Zanzibar kama ambavyo kimeanza katika kusaidia Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA).
Dkt.Mwinyi amezungumza hayo leo tarehe 14/9/2022 Mjini Unguja katika ufunguzi wa kongamano la Maji Zanzibar linalofanyika katika Hotel ya Golden Tulip mjini hapo, ambapo amekitaka chuo cha Maji kufunga mfumo wa kisasa wa kuendesha shughuli mbalimbali za Mamlaka hiyo unaojulikana kama Integrated Leakage Magagement System (ILMS).
Naye Mkuu wa Chuo cha Maji Dkt.Adam Karia alielezea mfumo huo na namna ambavyo umeleta ufanisi kwenye Mamlaka ya Maji Zanzibar.