Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mama Mariam Mwinyi amehani familia ya Marehemu Shomari Khamis Shomari nyumbani kwao Jang’ombe tarehe: 02 Januari 2024 aliyezikwa tarehe 31 Disemba 2023 Makaburi ya Mwanakwerekwe.
Marehemu Shomari Khamis Shomari ni ndugu wa Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Bi Zainab Khamis Shomari.