Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Balozi wa Qatar nchini Tanzania, Mhe.Fahad Rashid S Ali Marekhi aliyefika kwa mazungumzo Ikulu Zanzibar tarehe 05 Disemba 2023.
Katika mazungumzo yao wamegusia uhusiano uliopo kati ya Zanzibar na Qatar pamoja na fursa mbalimbali zilizopo Zanzibar ikiwemo uwekezaji, biashara, utalii,uvuvi, mafuta na gesi pamoja na huduma za kijamii hususani elimu na afya.