Home Kitaifa RAIS BIASHARA UNITED AWAITA WANACHAMA WAKE KUWA WAMOJA NA KUHAKIKISHA TIMU INAPANDA

RAIS BIASHARA UNITED AWAITA WANACHAMA WAKE KUWA WAMOJA NA KUHAKIKISHA TIMU INAPANDA

Na Shomari Binda-Musoma

RAIS wa timu ya Biashara United Revocatus Rugumia amewataka wanachaama wa timu hiyo kurudi kuwa wamoja na kushirikana ili kupanda na kurudisha umoja.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na wanachama hao kwenye kikao cha pamoja cha kujadiliana masuala yanayohusu timu hiyo.

Amesema pasipo kuwa na umoja na mshikanano hajuna jambo lolote la mafanimkio ambalo linaweza kufanikiwa.

Rais huyo wa timu amesema taarifa za umoja uliokuwepo siku za nyuma za ushirikiano wa wanachama unapaswa kurejeshwa na kusonga mbele.

Amesema kuja kwake kuungana na wanachama kuipeleka timu kwenye malengo yaliyokusudiwa na hilo litafanikiwa iwapo kutakuwa na ushirikiano.

Kikao hiki ni muhimu kwetu tunapoelekea mzunguko wa pili wa Championship na ili tuweze kufikia malengo yakupanda na kikubwa ni kuwa na ushirikiano.

Mimi kwa nafasi yangu kama Rais wa timu nipo tayari kutimiza wajibu wangu ili kufikia malengo na naomba kwa upande wa wanachama tuweze kushirikiana”,amesema.

Amesema kikubwa yale ambayo yamezungumzwa na kwenda kufanyiwa kazi na kuwataka wanachama kusamehana na kurudisha umoja wa kusaidiana na kukutana mara kwa mara.

Daniel Stephen mmoja wa wanachama wa Biashara United ameshukuru kufanyika kwa kikao ambacho kimekuja na maono ya kurudisha umoja uliokuwepo.

Amesema Biashara Jamii ndio mfumo ulioweza kuisaidia timu hiyo na sasa umefika muda muafaka wa kurudi na kuwa wamoja na kurudisha upendo.

Melvin Nashon kwa upande wake kama mmoja wa wanachama pia amesisitiza kikao cha kuchagua viongozi wa umoja kifanyike mapema ili yaliyokusudiwa yaweze kufanyika.

Wakati huo huo kesho timu ya Biashara United itaikaribisha timu ya Mbuni fc kwenye mfululizo wa michezo ya ligi ya Championiship kwenye uwanja wa Karume huku mashabiki wakiombwa kujitokeza kuisapoti timu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!