Na Magrethy Katengu
Bodi ya Umma Manunuzi na Ugavi imewapiga marufuku Wataalamu wanaofanya kazi za Manunuzi na Ugavi za serikali ikiwa hawajasajiliwa na yeyote atakayebainika yuko kinyume sheria itachukuliwa dhidi yake.
Agizo hilo limetolewa leo Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Manunuzi na Ugavi (Psptb) Godfred Mbanyi ambapo amesema Wizara ya Fedha na Mipango inaendelea kukamilisha wa Mfumo mpya hivyo kabla ya kuanza kufanya kazi bodi watakwenda kufanya ukaguzi katika taasisi, Ofisi zote za serikali na ikibainika kuwa kuna mtu ameajiriwa kufanya kazi hiyo na hana sifa stahiki mwajiri aliyemuajiri atawanibika kisheria .
Sanjari na hayo amesema hapo awali kulikuwa na madhaifu mengi ambayo yalikuwa yakitokea kupitia mfumo wa zamani sababu wataalamu ambao waliokuwa hawana sifa stahiki kufanya shughuli hizo na kusababisha madhaifu ambayo Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali akija kukagua anakuta hasara hivyo jambo hilo halitavumiliwa linakwenda kutafutiwa mwarobaini.
Mtaalamu yeyote hata Kama ni Afisa Manunuzi mwandamizi ana cheo kama hana usajiliwa na bodi hii Psptb hatoweza kutoka kwenda hatua moja nyingine kufanya kazi hatoweza kama hajaainisha taarifa zake za usajili katika mfumo huu mpya hivyo tunapofanya ukaguzi tukimbaini Mwajiri aliyemuajiri atawajibika kisheria “amesema Mbanyi
Hata hivyo mfumo huo upo kwenye majaribio na wote watakaokuwa katika usajili wa Mfumo mpya itasaidia kutoa huduma kwa urahisi bila kuchelewesha kazi za serikali hivyo nawasisitiza Waalamu wote wa Manunuzi na Ugavi kujisajili mapema .
Hata hivyo amesema ikitokea taasisi,Ofisi yeyote ya serikali Maafisa wake hawajasajiliwa na Mfumo huo mpya sheria Kali zitachikuliwa kwani hapo awali kabla ya mfumo huo mpya kulikuwa na changamoto ambapo hata ambao siyo wataalamu wasio na sifa ikiwemo taaluma usajili walikuwa wakitumia mfumo na kusababisha taarifa za Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali akikagua kukuta mapungufu .
Aidha Serikali mpaka sasa inaingia gharama ya kujenga mfumo huo mpya wa Manunuzi na Ugavi na inakwenda kukamilika hivyo utasaidia kurahisisha huduma na kuwatambua wataalamu wote wanaofanya kazi hiyo ambao wana sifa stahiki.